Member of EVRS

Friday 4 May 2012

Rwanda: Ukatili Bado Unajitokeza Hapa na Pale

Ukatili wa mtu, wakati mwingine upo kwenye damu yake.
Sio lazima iwe kulipiza kisasi.

Kama huyu kijana wa kinyarwanda mwenye umri wa miaka 12 ambaye alirudi nyumbani na kudai apewe chakula, lakini dada yake wa tumbo moja mwenye miaka 10 alimueleza ya kuwa chakula hakijawa tayari.
Huyu kijana kwa hasira zake, akalifuata jembe na kumkata kata dada yake mpaka akafa, hakuishia hapo, akaanza kumkata na mdogo wake wa kiume wa mika 4 na kumjeruhi vibaya kabla hajadhibitiwa.


Msemaji wa polisi, alisema tukio hili linawakumbusha watu ya kuwa wanahitaji kutoa ushauri na nasaha kwa vijana, japo kwa huyu sijaelewa kwa nini alifanya hivi, kwani alizaliwa miaka mingi tu baada ya mauaji ya kimbari!

Katika tukio jingine la ukatili ni la huyu baba asiye na utashi wa kutunza watoto wake, pale alipokodisha muuaji aue watoto wake wawili wa kuzaa tena wakiwa wadogo wa umri wa miaka 6 na 8
Mtu aliyekodishwa kuwaua watoto hao aliahidiwa kupewa kiasi cha faranga za Rwanda 80,000 ambazi ni karibu ya shilingi 200,000 za kitanzania. Muuaji mtarajiwa alikubali kuwaua japo nia yake ilikuwa kuwaokoa kama anavyodai mwenyewe! Kwa hiyo alipopewa kianzio, aliamua kutoa taarifa polisi juu ya tukio hilo ambapo mtuhumiwa alikamatwa.
Baadaye ilikuja kujulikana sbabu ya kutaka kuwaua watoto hao ni Mama wa watoto hao kudai vyombo vya sheria vimshughulikie huyo baba ili atoe fedha za matumizi ya watoto hao na kama hawezi, basi apewe sehemu ya ardhi ili aitumie kuwatunzia watoto hao wawili. Pia ilikuja kujulikana ya kuwa mama wa watoto hao, ni mke mdogo kwa mtuhumiwa huyo!
Huyu jamaa aliona njia nzuri ya kutokuwa muwajibikaji wa kutunza watoto wake ni kuwaua!

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ama kweli nimeamini si lazima awe mtu wa baki. Ila jamani kweli mtoto wa miaka kumi na mbili kumuua dada yake ambaye wamepishana miaka 2 tu. Kwa akili yangu lilikuwa si jukumu la dada huyu kumwandalia chakula kakake. ndio najua Nyumbani Afrika mtoto kuanzia miaka 6 na kuendelea anaweza kutunza familia. Lakini mweeh!!

Rachel Siwa said...

Mmmhh hawa watu bwana mimi nawaogopa sana.Hata Amani ya huko pia siiamini kaka yangu uwe makini.Mungu awasimamie sana.