Member of EVRS

Sunday, 6 May 2012

Yanga Yawapa Ujiko Simba

Pazia la ligi kuu ya Tanzania limemalizika leo.  
   
Moja ya mechi iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka ilikuwa ni kati ya Bingwa mpya wa msimu 2011/12 Simba ya Dar es Salaam na mabingwa waliopita wa msimu wa 2010/11 Yanga ya Dar es Salaam pia. 
   
Mpira ulipoisha, Yanga walikuwa wamefungwa mabao 5 - 0, huku magoli 3 yakiwa yamefungwa kwa adhabu za penati!  
   
Hivyo Yanga wamemaliza msimu kwa kuwapa ujiko na sifa timu ya Simba ambapo timu zitakazokuja kucheza na Simba zitakuwa zinatishiwa na ushindi huu wa kufungia ligi kuu ya Tanzania Bara.

No comments: