Member of EVRS

Tuesday, 8 May 2012

Makinda: Tanzania Haijawa Tayari Kuridhia Kuondolewa kwa Masharti ya Uhamiaji EAC

Mkutano wa viongozi wa mabunge (National assembly speakers) ya nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaokutana jijini Kigali, Rwanda walikuwa na mjadala mkali unaohusu kufungulia mipaka na kelegeza masharti ya uhamiaji kati ya nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Habari zinadai ya kuwa mashambulizi mengi yalielekezwa kwa Tanzania kwani bado haijaridhia kufungulia mipaka yake kama nchi nyingine zinavyopenda kuharakisha mkataba huu.
   
Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda alisema kwa sasa Tanzania haipo tayari kufanya hivyo kwa kuwa wananchi wa Tanzania wanatakiwa kuulizwa kwanza kama wapo tayari kufanya hivyo ukizingatia ina idadi kubwa ya watu kuliko nchi zote za Afrika Mashariki. Pia aliongeza kusema ya kuwa kumekuwa na wahamiaji haramu wengi wanaoingia Tanzania kutoka nchi mbalimbali hata zilizo nje ya Afrika mashariki ambao huleta vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani ndani ya Tanzania. Kwa hiyo kuna haja ya kudhibiti hilo kwanza. 
  
Kingine alichoongeza Mama Makinda, ni kuwa Tanzania haina vitambulisho vya taifa, na kwa sasa iko kwenye mpango wa kuvitoa kwa wananchi, na hatarajii zoezi hilo litakwisha mapema, labda litachukua zaidi ya miaka miwili kutoka sasa.

No comments: