Member of EVRS

Friday, 25 May 2012

Jihadhari na Bidhaa Kutoka China

Kwa siku nyingi kumekuwa na malalamiko kutoka nchi zinazoendelea kuhusiana na uduni wa bidhaa kutoka China. 
Serikali ya China ilikuwa inajitetea na kusema inaudha bidhaa zake kutokana na mahitaji ya wateja, maana yake nchi zinazoendelea zilikuwa zina agiza bidhaa za bei nafuu lakini zikiwa na ubora duni. 
Serikali ya Tanzania kupitia mamlaka zake, ilikuwa inazikamata bidhaa bandia na kuziteketeza. Jitihada hizi hazijaweza kuzimaliza bidhaa bandia au feki au zenye ubora wa hali ya chini.  
   
Wiki iliyopita, Serikali ya Marekani ililaumu China kwa kuiuzia vifaa vya ndege za kivita ambavyo takribani asilimia 60 ya vifaa vilivyotumika kutengeneza ndege za kijeshi, vilikuja kugundulika kuwa vilikuwa chini ya kiwango.  
 
Uchunguzi uliofanyika na taasisi za Marekani kwenye bidhaa nyingine zilizoingizwa nchini humo zikiwamo nguo, baiskeli nk umebaini ya kuwa bado wanatengeneza na kuzipeleka bidhaa bandia zenye ubora hafifu wakati mwingine kwa asilimia 90 ya bidhaa zote wanazoziingiza Marekani, japo wanabandika alama au lebo sahihi. Watu wamejikuta wakinunua lebo sahihi huku bidhaa ikiwa bandia.
  
Baadhi ya taasisi zimeshindwa kuyafunga maduka au kuteketeza bidhaa zilizouziwa bidhaa bandia kutoka China kwani wanahofia kuwa kuna mamilioni ya watu watapoteza ajira wakati kuna kiu kubwa ya ajira kwa watu wengi! 
  
Habari zipo nyingi, lakini unaweza kusoma mojawapo hapa

No comments: