Member of EVRS

Friday, 16 April 2010

Mlipuko Wa Volkeno Iceland Waleta Usumbufu Mkubwa Ulaya na Kwingineko

Kufuka kwa moshi na vumbivumbi la volkeno iliyolipuka huko Iceland kumesababisha hasara kubwa kwa mashirika ya ndege huko Ulaya kaskazini magharibi baada ya kufuta safari nyingi za kuruka na kutua kwenye viwanja vilivyoko huko baada ya moshi mzito wa volkano hiyo kutanda angani.
Hali hii imesababisha hofu kwa mashirika ya ndege kupita karibu na moshi huo ambao unahofiwa unaweza kuingia kwenye injini za ndege aina ya jet na kuweza kusababisha mlipuko au kuzimika ghafla kwa injini hizo na hivyo kusababisha kuanguka kwa ndege.
Wataalamu wa masuala ya jeolojia na afya wameshauri watu wakae ndani pale vumbi hilo litakapoanza kuanguka chini maana linaweza kuwa na madhara kiafya.


Picha juu: Abiria waliokwama wakiwa wamejipumzisha kwenye vitanda vya dharura uwanja wa Frankfurt, Ujerumani wakisubiri maelekezo zaidi


Habari kutoka msnbc

5 comments:

jaz@octoberfarm said...

hi chib! i was just thinking about you a few days ago. i see you have been traveling! i hope all is well with you! welcome back to blogland! joyce

Upepo Mwanana said...

Poleni ndugu zetu. Naona Africa imesalimika kwa majanga haya ya asili

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wewe uoni mafuriko na vimbunga????

naomba kuuliza kama volcano ina uhusiano wowote na gulobally woming a.k.a climate change. kuuliza si upumbavu, bali harakati za kuondoa ujinga na upuuzi kichwani

chib said...

@ Kamala, mie sina ujuzi sana na mambo ya jeolojia, kwa kutokujua kwangu, nafikiri labda hakuna au upo kidogo sana. Waatalamu wanaweza kutusaidia

Yasinta Ngonyani said...

tuombeane ndicho kilichobaki!