Member of EVRS

Monday, 26 April 2010

Miaka 46 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Leo watanzania tuna adhimisha miaka 46 ya kumbukumbu ya muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar ambao ulizaa Tanzania yetu ya leo.

Muungano huu haukuzaliwa kwa kujifurahisha au kuwafurahisha watu au mataifa fulani.
Ulipoanzishwa ulikuwa na malengo mengi.

Kwa sasa tunaelekea kukaribia nusu karne ya muungano huu, lakini sidhani kama tulishawahi kukaa na kutafakari mambo mangapi tumeyatimiza kutokana na madhumuni au makusudio ya muungano huu.

Nina imani viraka katika muungano huu ni vingi sana kiasi kwamba tunaanza kusahahu rangi halisi za muungano wetu.

Si vibaya tukianza kutafakari na kuufanya muungano huu uwe bora na wa mshikamano zaidi.

Mungu ubariki Muungano wetu, Mungu wabariki Watanzania.

1 comment:

Fadhy Mtanga said...

Naungana nawe kaka Chib. Ni kweli uyasemayo. Nami kibarazani kwangu nimeandika kuhusu muungano. Karibu sana.