Sifa kuu ya kiongozi wa kiserikali hapa Rwanda, ni kuwa kuwa muadilifu.
Njia ya kuhakikisha ya kuwa wewe ni mtu safi, mara uteuliwapo au kuchaguliwa na wananchi katika bunge, ni lazima utangaze mali zako zote, na zoezi hili hufanyika kila mwaka.
Kwa sasa serikali ya Rwanda inataka kukomesha masuala ya ufisadi, kwa hiyo imetunga muswada wa sheria wa kuwabana viongozi wasiotaja mali zao ya kuwa serikali italazimika kuzitaifisha.
Muswada huo umeshafikishwa bungeni, na kama utapitishwa, mafisadi wote wa Rwanda watakumbana na kizingiti.
Ningefurahi sana kusikia siku moja watuhumiwa wa ufisadi wote Tanzania wanataja mali zao hadharani. Labda na sisi tungepungukiwa na mafisadi.
Kuiga sio ugonjwa, Tanzania inapaswa kuiga mfano huu
1 comment:
Kwani serikali ya Rwanda haiwezi kuhamia Tanzania, I mean Rais wa Rwanda?
Post a Comment