Member of EVRS

Monday 11 January 2010

Ombaomba Wanapohamishia Ofisi Kanisani!

Jana nilienda kanisani kwa ajili ya ibada. Watu waliuwa wengi kuliko siku nyingine za kawaida, achilia mbali siku za sikukuu kama krismasi na siku za pasaka ambapo ndipo watu wengine humkumbuka Mungu au labda kuja kuonekana/kujionyesha :-(

Mbali na mahubiri mazuri ya Kasisi, kulikuwa na tukio lililojitokeza kabla ya ibada, pale mlalahoi (ombaomba) mmoja alipoingia kanisani, sio kwa ajili ya ibada, bali kwa ajili ya kupiga mizinga (kuomba). Kwa mshangao watu walikuwa wakimcheka kicheko cha tumboni(kimyakimya) pale alipokuwa ananyoosha kiganja chake kuomba.

Baadaye alipotoka nje ya kanisa, kulizuka mrindimo wa minong'ono kutoka kwa watu huku wakiendelea kukenua "magego".

Kingine kilichonishangaza ni pale ibada ilipoisha, kuna baadhi ya watu walitoka nje ya kanisa na kuanza ubishi hapohapo wa ligi kuu ya mpira wa Uingereza, washabiki wa Man U walikuwa wamenuna kwa sare ya jumamosi huku wa Chelsea wakiwa na bashasha!

Sasa sijui kujazana kanisani ni kuja kusali au ni sehemu ya makutano!

3 comments:

Faith S Hilary said...

watu wanaenda kanisani for all sorts of reasons...kusali, kukutana na watu ambao hujawaona the whole week, kutafuta wachumba etc.

Ila mimi naona ombaomba anyeingia kanisani au akiwa kwenye mandhari ya kanisa anakuwa ananinyima raha kwa "kunisuta" kwamba naingia kanisani na sijampa kitu. Mimi mwenyewe unajua una kiasi gani na kiasi gani natoa "KANISANI" kwa ajili ya "SADAKA". Wengine sijui mtasemaje lakini mimi ananinyima raha kusema ukweli. Though it is not a funny matter.

Yasinta Ngonyani said...

Inawezekana vyote kusali na pia ni sehemu ya makutano.

Christian Bwaya said...

Kuna siku jamaa yangu mmoja alikuwa akidai vijana wengi siku hizi wanafanya maigizo kanisani. Mie nilimwambie bora wakafanye maigizo hayo kanisani kuliko kufanya kweli mtaani.

Kwa hili Chib, mie naona bora hata kuna watu wanafanya kanisa kuwa sehemu ya miadi. Nayo ni hatua. Very positive.