Member of EVRS

Friday, 18 December 2009

Ukara: Kisiwa kisichojulikana sana Tanzania

Kisiwa cha Ukara, ni moja ya visiwa vilivyoko katika ziwa Victoria au Nyanza katika nchi ya Tanzania.
Wenyeji wa kisiwa hiki wanaitwa Wakara.
Si watu wengi wa Tanzania wanaoifahamu jamii ya wakara, hata wakati mwingine Mkara akijitambulisha kwa kabila, kuna watu humuuliza kabila hilo lipo nchi gani!!

Kisiwa hiki kiko kaskazini ya kisiwa kingine kikubwa kabisa katika ziwa hili kiitwacho ukerewe.
Ukara ipo karibu kabisa na mstari wa ikweta, kama nyuzi moja tu kusini mwa ikweta.
Wenyeji wa kisiwa hiki ni waungwana sana, na shughuli kubwa ya kwao ni uvuvi na kilimo.

Kama waafrika wengine, mila na tamaduni zao si tofauti sana na wengne. Mambo ya nguvu za asili pia yapo kwa baadhi ya wenyeji, na wakati mwingine watu huwaogopa kwa mambo ya kauchawi, lakini chumvi hukolezwa sana.

Wakara wanasifika kwa uaminifu na kufanya kazi ngumu kwa bidii hasa wanapokuwa nje ya kisiwa chao, na hata zamani walikuwa maarufu kwa kubeba mizigo sehemu za mjini hasa Mwanza, kiasi kwamba walikuwa wanawatania watu wote wabebao mizigo kuwa ni wakara.

Kivutio maarufu kisiwani huko, ni jiwe ambalo linaweza kucheza lenyewe baada ya kuamriwa na watu wenye uwezo wa kufanya hivyo.

Historia inadai jiwe hilo miaka kama 40 na ushee iliyopita lilikuwa nchi kavu, na watu walikuwa wakipeleka watoto mapacha au walemavu kuuwawa, maana walikuwa wanachukuliwa kama mkosi katika familia. Pia lilikuwa ni jiwe maarufu la matambiko. Kutokana na mvua kubwa zilizonyesha, maji yaliongezeka, na kufanya jiwe hilo lizungukwe na maji.

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

mie ndo kwanza nakisikia sikuwa na taarifa kama kuna kisiwa kiitwacho Ukara. Ahsante sana kwa taarifa hii hizi blogu ni safi sana watu kila siku tunajifunza jipya. Pia nakutakia mwisho wa juma hili uwe mzuri.

Anonymous said...

Duh, wabongo na jiografia mbalimbali.

SIMON KITURURU said...

Sikuwahi kukisikia. Hivi huko sio alikojificha Bin Laden?:-)

chib said...

Hiki ni kipimo tosha...
Nilifikiri waliokuwa hawakijui ni....
@Simon :-)
Ukitaka kuwajua watu wa huko wanafananaje, basi tafuta picha yangu, maana mimi ni nakala halisi ya huko visiwani

രഘുനാഥന്‍ said...

Dear friend

Wish You a Merry X'mas and Happy New Year

chib said...

Dear friend with difficult name to read, thank you so much, again I wish you the same