Member of EVRS

Tuesday, 29 December 2009

Airports Inspection! Beyond the Imagination

Should we say ....... let those who doesn't value human life be blind instantly!!

Pamoja na kuwa Viwanja vingi vya ndege hasa bara la Ulaya na Marekani vimekuwa vikichukuwa tahadhari kubwa na kufanya upekuzi mkubwa kwa abiria kuhakikisha usalama wa safari za ndege na abiria wake.

Wasafiri wengi wamekuwa wakilalamikia namna wanavyopekuliwa na hasa unapoonekana kwa kudhaniwa na wewe ni gaidi. Mpapaso ndio unaolalamikiwa na watu, maana umezidi kipimo, na mabegi ya mkononi kumwagwa na kupekuliwa kila kitu. Pia mbwa maalum wamekuwa wakitumika katika ukaguzi huo

Pia kumekuwa na muda mrefu wa ukaguzi kabla hujapewa ruhusa ya kuendelea na safari ya kuwa upo salama kwa watu wengine.

Vyombo vya ukaguzi wa mwili kwa kutumia mionzi maalumu ambayo inawekumulika mwili wote imekuwa inatumika, ambapo mkaguzi hukuona karibu kila kitu kama vile uliyevua nguo zote!

4 comments:

jaz@octoberfarm said...

hi chib! i am so happy to hear from you again! how was your holiday? joyce

Halil Mnzava said...

Ni kweli ukaguzi umekuwa mkali sana,wakati mwingine kuwa kama kero lakini nadhani kwa mazingira ya sasa ni kwa nia njema.

Kaka nakutakia heri ya mwaka mpya wenye mafanikio na afya tele.

Yasinta Ngonyani said...

Kuna wakati nimekuwa najiuliza ukaguzi wote huu lakini hata hivyo watu ni wajanja tu sijui huko tuendeko itakuwaje? Haya Chib zimebaki siku chache kuweka malengo ya mwaka 2010...LOL

Anonymous said...

What a powerful sentence in the beginning. assume the remaining writing to be as impressive, yet trying to figure out the language.
Please have a wonderful Wednesday.