Member of EVRS

Thursday 5 November 2009

Tanzania: Hatuna Wabunge!


Katika habari iliyonishangaza leo ni pale niliposikia baadhi ya waheshimiwa wabunge wa Bunge tukufu la Tanzania wakipendekeza ya kuwa watoto wa kike wasinyimwe uhuru wa kuolewa wakati wowote wanapojiona wako tayari kwa masuala hayo hata kama wako chini ya miaka 18.

Mbunge mmoja alidiriki kusema ya kuwa utakuta kabinti kazuri ka miaka 16 kapo tayari ....., awali alikuwa amedai watoto wa miaka 14-15 kukataliwa kuolewa ni kunyimwa haki yao ya msingi!!

Na pia... ati si kila mtoto ana mpango wa kuendelea kusoma baada ya kumaliza elimu ya msingi.....

Nawashukuru wale wabunge waliopinga kauli hizi.

Pata habari zaidi HabariLeo

5 comments:

John Mwaipopo said...

with this house in which any boob can get into as long as he/she has moola what do you expect?

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli sasa tunakokwenda ni kubaya kabisa. Mtoto wa mika 14-15 kuolewa, wakati mwenyewe anahitaji msaada kutoka kwa baba na mama wa kutunza je huyo ataweza kweli kutunza nyumba/mume? Kwa nini kama hawataki kusoma wasihamasishwa yaani kwa kweli bado tupo na misingi ile ile ya kusema kumsomesha mtoto wa kike ni kumaliza pesa tu. Inasikitisha sana kuona bado iko hivi.

Anonymous said...

Cha kusikitisha zaidi, ni kuwa wabunge tena ndani ya bunge rasmi kutoa kauli za kiwewese kama hizo. Cha kushangaza waliokuwa wanaunga mkono ni wanaume na wanawake!!

Simon Kitururu said...

Tukumbuke lakini kuwa Makabila mengi kipimo cha kuwa KIGOLI kafikia kuweza kuolewa sio UMRI kwa kuwa MIAKA kwa makabila mengi ni jambo lililokuja juzijuzi tu.

Kipimo halisi kitumikacho kienyeji kujua mtoto anaweza kuhimili NANIHII au ndoa, kwa kawaida huwa ni saizi ya titi nau tu ni kuwa Kigoli kavunja ungo.

Kwa hiyo wale VIGOLI wenye kuvunja ungo haraka na na kuota chuchu wakati umri mdogo walikuwa wanaolewa katika umri mdogo sana tokea zamani. Na kumbuka kuna akinadada ambao wanawahi sana kuvunja ungo na kinachofuati ni Wazazi kuogopa kuwa KIGOLI baada ya kuvunja ungo kama kawaida ataanza kuwashwa kikubwa kwahiyo ATAKUNWA KIKUBWA ,na kwa hilo anaweza akapata mimba na kutia aibu familia.

Ku -solve hilo - preemptive action iliaminika ni kumuoza kwa lidume limendealo ngoma mpya wakati huo hata kama sura ni kama trekta.

Na kuna uwezekano wabunge wengi tulionao sio generation zaidi moja au mbili kutoka fikira za kienyeji nilizoziainisha hapo ju au tu -kutoka katika swala la kuamini kuwa muoze binti mapema kwa kuwa ndiye apataye mimba na kutia familia aibu.

CHAKUSIKITISHA tu ni kwamba hawa wabunge ndio wanaotakiwa wawe na upeo wa kubadili jamii mawazo kuhusu swala hili la kujali watoto wa kike na kustukia mtoto ni mtoto - na kazi ya wakubwa mojawapo ni kuelekeza watoto na si kwa kuwa wameota TITI na wanawashwa kikubwa basi jawabu la hilo ni kuwaoza tu.

Na kama wapo watoto wasiopenda kwenda shule basi na watoto wa kiume katika hilo wamo.

mdoti Com-kom said...

tatizo la wabunge ni uduni uliotamalaki ambao wao wanauita utamaduni ;lakini si kweli kuwa wanauelewa wowote wa kibiologia au kiafya kwa ujumla hata kisaikolojia' wangeyajua hayo wasingethubutu kuropika. labda qualifikation za ubunge zibadilishwe