Member of EVRS

Tuesday, 17 November 2009

Gaddafi Atoa Mpya Italia

Click red letters below this message for English information

Kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi akiwa Rome Italia aliandaa party kwa kuwaalika akina dada zaidi ya 200 wa kitaliano kwenye sherehe ambapo hao akina dada walilipwa kiasi cha USD 75 kuhudhuria sherehe hiyo.

Kampuni moja ya kuandaa warembo ilipewa tenda hiyo na kuwakusanya mabinti hao kwenye hotel iliyopangwa, ingawa kuna baadhi waliachwa kutokana na mavazi yao ambayo yanadaiwa hayakuwa ya heshima, pia kuna baadhi waliachwa kwa sababu walikuwa wafupi!

Badala ya sherehe, Gaddafi alipofika alianza kutoa mhadhara ambao ulichukua kama dakika 45 wa kuwaeleza hao mabinti warembo kuhusu uislamu na mchango wa wanawake katika dini ya kiislamu, pia kuanguka kwa dini ya ukristo na wanawake kugeuzwa watumwa wa mapenzi kwa wanaume kwenye nchi za magharibi, na mwisho kuwataka wabadili dini na kuwa waislamu.
Pia alitoa zawadi ya kitabu kitakatifu cha dini ya kiislam (Quran) na kitabu chake cha maarufu cha kijani kikiwa na semi zake za busara kwa washiriki wote.

Baada ya hapo, Gaddafi alijichanganya mtaani na kuishia kwenye mgahawa wa wazi kupata chochote.

Read more here and here

7 comments:

Fadhy Mtanga said...

Duh! Huyu jamaa nashindwa nimwelezeaje, zaidi ningesema, huwa ananishangaza daima.

Thom said...

Very strategic man

Born 2 Suffer said...

Huyu anazake peke yake yani.

John Mwaipopo said...

i think scientists need to examine his brain when he dies. he is an unusual dictator trying to use Quran to justify his bloody hands.

John Mwaipopo said...
This comment has been removed by the author.
Anonymous said...

He want to be the first president of United States of Africa

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ni bonge la mtu. sasa yeyekama anaona uisilamu ni mzuri na labda ndio maana kafanikiwa kuwa dictator wa kulisha vizuri watu wake, kwa nini asiutangaze? na kila kitu kama vile dini husambaa zaidi kwa kupitia uzazi wa mwanamke, ni bonge la mtizamo na anaweza fanikiwa huyu jamaa