Member of EVRS

Friday, 13 November 2009

Plane accident at Kigali airport


Ndege ndogo ya kampuni ya Rwandair kama inavyoonekana hapo juu, jana ilipata tatizo muda mfupi tu wakati ilipokuwa imepaa kwa tatizo ambalo rubani hakulitambua hivyo kulazimika kushuka.

Wakati akiwa amefika sehemu ya kupaki, aliripoti ya kuwa ndege imekataa kuzimika na kuwa bado injini zina mwendo kasi na hivyo alilazimika kufuata ukingo uliopo katika uwanja wa Kimataifa wa Kigali, lakini aliugonga uzio huo na ndege kupitiliza, na kisha kujigonga katika ukuta wa jengo la airport sehemu ya wageni mashuhuri (VIP lounge) kiasi kwamba sehemu ya mbele ya ndege kuingia katika jengo hilo.

Abiria mmoja amefariki na wengine 10 kujeruhiwa. Wafanyakazi wote wa ndege wapo salama.

Ndege hiyo yenye umri wa miaka 10 ilikuwa ikielekea Entebbe, Uganda

Habari zaidi zinadai ndege hiyo ilifutwa usajili wa kuruka huko USA mwaka 2004, na kuuzwa mwaka 2007.

For more information read here and here

11 comments:

Faustine said...

Shukrani kwa kutuhabarisha.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa habari.

John Mwaipopo said...

JetLink Express watuambie kwa nini walinunua ndege mbovu ambayo ishapigwa marufuku kubeba watu. na pia kwa nini waliuza kitu hatari.

Rwandair Express nao watujibu maswali mawili. mosi kwa nini walinunua ndege pasi na uchunguzi kamili wa kitaalamu. pili kwa nini walipakiza abiria (na wafanyakazi wa ndege)

Hivi hizi za kina Precision air na washindani wake tunajua historia zao au tunafurahia rangi na ulimbukeni wa kupanda ndege. Au tutajua kuwa zilishapigwa marufuku ulaya na marekani baada ya kuwatua watu ngorongoro wakiwa maiti badaya ya mwanza na bukoba wakiwa hai. kazi ipo!

John Mwaipopo said...

shida ya ndege ni kupaa tu lakini kutua itatua tu hata kwa namna hatarishi. asante kwa taarifa ya kusikitisha

Anonymous said...

Ufisadi hata kwa maisha ya binadamu!!

chib said...

Inatisha hii. Matatizo ya kununua ndege za mtumba

SIMON KITURURU said...

:-(

Halil Mnzava said...

Duh,hii kali!Ufisadi ufisadi kila mahali?sasa labda tutafute asili ya ufisadi kisha tuteketeze mbegu yake maana mhh!!!

Mzee wa Changamoto said...

Kinachonitisha ni hapo mwisho unaposema "Habari zaidi zinadai ndege hiyo ilifutwa usajili wa kuruka huko USA mwaka 2004, na kuuzwa mwaka 2007."

Lakini hili lisingenitisha kama viongozi wetu wangekuwa wanawajibika kwa makosa yao. Na kama wangekuwa wanatuhabarisha yatokeayo. Leo hii HABARI MUHIMU kwa mTanzania si HAKI bali ni offer. Sasa sijui ni nani anayeweza kwenda kuhakikisha kuwa kina "Air Changamotos" zinazomwagwa nyumbani zina viwango vya kuruka a sio kwa kuwa hawawezi hata kuzi-recycle?
Vinavyotuua vingi na wawajibikaji hakuna
Labda tujipange kuwauliza wenye mamlaka nyumbani kuhusu hizi "brand new second hand" tuonazo.
Blessings

chib said...

@Mzee wa Changamoto. Umesema hapoo

Bennet said...

Hizi nchi zetu za Afrika zina fanana sana kitabia