Member of EVRS

Saturday, 28 November 2009

Ulevi huu.... Haufai Kabisa
Kuna mlevi mmoja alitoka kwenye sherehe ya kumkaribisha bosi wao mpya ambayo iliisha kwenye muda waa saa 4 usiku. Kwa kuwa kulikuwa na pombe za bure, alizifakamia kwa spidi ya Usain Bolt, na mara akawa taabani.

Baada ya sherehe kufungwa, waliondoka, na yeye kuona bado ni saa 4 tu, akajishauri kupitia baa ya kijiweni ili kufukuzia harufu kabla ya kwenda nyumbani.

Kwa mtazamo wake, alipofika kwenye "baa" yake maarufu alijitoma ndani na kukaa kwenye kiti saafi, na kumwagiza mtu aliyemuona kama muhudumu kwa kejeli na t's*

Mlevi: kilimanjaro baridi haraka wee @O*'\".

Muhudumu huku akicheka kwa kejeli akaenda kumchukulia maji ya kilimanjaro.

Huku nyuma, akabaki binti wa miaka 15 hivi, na mlevi akarusha neno....

Binti akamshangaa, na kuondoka karibu yake.

Mlevi kuona anakosa alichotaka .... akamwamwambia huyo binti

Mlevi: Ati we binti unanikimbia, hujui ya kuwa jana tu nimelala na mama yako

Mara "muhudumu" akarudi na maji, na mlevi akawa anajiandaa kuporomosha tusi kwa kuletewa maji badala ya bia, lakini kabla hajafunua domo lake.... mhudumu alishasikia yote kwa bayana kauli ya huyo mlevi. Akamwamuru Mlevi, tafadhali Baba Pasua, naona umelewa sana, ingia chumbani ukalale. Mambo mengine tutaongea kesho.

Mlevi kwa ghafla akahisi kama kapigwa na radi vile......

Kwa ufupi, Mlevi hakuwa baa kama ulevi ulivyomdanganya, alikuwa amefika nyumbani kwake. Muhudumu ni mkewe na binti ni mwanaye.

Tafakari ujumbe huu, na nakutakia weekend njema

12 comments:

Faustine said...

......Hii ni hatari!

Candy1 said...

Sad but funny...Pombe should be illegal...what do you think? lol probably nitashambuliwa hehehehe

Yasinta Ngonyani said...

Kweli pombe ni hatari, Kama wengine wasemavyo ukinywa pombe unachafua akili. Hii sasa kali mpaka anashindwa kumfahamu mkewe?!!!

Fadhy Mtanga said...

Maweeee!
Kaka Chib umeniacha sina mbavu. Inachekesha, lakini inafikirisha.

SIMON KITURURU said...

DUH!

@Candy ! : unataka kuniua nini kwa kushauri pombe iwe iligo!:-(

Anonymous said...

Yaelekea alifakamia the kick au Bia Bingwa, ndio huwa zinaondoa kumbukumbu namana hiyo. He he he

mumyhery said...

Pombe si maji

Kachupa said...

Candy! Serikali itapoteza kodi nyingi kama alcohol ikiwa iligo.
Halafu unafikiri tutapunguza mawazo kivipi! Na vikao vitaendeshwaje bila vyupa?
@ Simon, tupo klabu moja. Zidumu bruwarizi zote, ila wanywaji wasiwe kama huyu mlevi :-(

Anonymous said...

Kwa ulevi wa namna hiyo, bora kustaafu

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mimi niliustaafu ulevi baada ya......

Kachupa said...

@KAMALA: ...baada ya kuingia baa kama ya mlevi huyo he heh hee

John Mwaipopo said...

we candy! ssshhhhhhhh.... noma. yu wanti asi ol ded eeh?

mara kadhaa huwa inatokea. tena mara nyingi ni hizi za bure au za ofa. akina sie tujijue kama ni 3 iwe hivyo, kama ni 4 iwe hivyo,kama ni 7 kama mimi iwe hivyo. ha! ha! ha!