Member of EVRS

Monday, 23 November 2009

Peru:Watu Wakamatwa kwa Kuuza Mafuta ya Binadamu


Photo: Peruvian police seized containers which was proven to contain human fat extracts

Wakati Tanzania tukiwa tunapigia kelele mauaji ya albino kwa kile wajinga wanachodai ni kupata utajiri wa haraka haraka kwa matambiko kibudu ya kupata bahati na mafanikio katika biashara, kwa wenzetu huko Peru wanaua watu, na kuwakata mikono, miguu na vichwa, kisha kuvining'iniza viungo hivyo na kuwasha mishumaa chini yake, na kutokana na joto la mishumaa hiyo, mafuta huyeyuka na kuchuruzika kwenye vyombo walivyotegesha chini na kisha kuuza lita moja kwa dola 15,000.

Mafuta hayo hutumika kama kipodozi kwa kuondoa mikunjo ya usoni a.k.a ndita za uzeeni (facial wrinkles) kwa wale wasiotaka kuonekana wazee hasa akina mama. Daktari mmoja wa ngozi aliyebobea katika matibabu hayo, amesema huwa wanatoa mafuta hayo kwa mgonjwa mwenyewe hasa sehemu ya takoni au tumboni, kwani kuchukua mafuta ya mtu mwingine kunaweza kuleta mzio (allergy) mbaya na inaweza kusababisha kifo kwa baadhi ya watu.

Mmoja wa watuhumiwa aliyekamatwa amesema amekuwa akifanya kazi hiyo ya kuua watu ili kupata mafuta ya binadamu kwa zaidi ya miaka 30. Na kwa mwaka huu karibuni watu wapatao 60 wamepotea kiaina.

Kwa habari zaidi au kwa kimombo for more information read here

8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

HAKIKA HUU NI MWISHO YA DUNIA KWELI, NDUGU ZANGUNI TUKAA NA TUJIANDAE! KAZI KWELIKWELI.

Yasinta Ngonyani said...
This comment has been removed by the author.
Anonymous said...

Unapovumbua kitu kimoja, wengine wanatumia uvumbuzi wako kujinufaisha kwa roho za wengine.
Na nyie vizee, kwa nini hamtaki kuzeeka, sasa ndio nini mnyofolewe matako eti ili muondoe makunyanzi ya uzeeni usooni.

SIMON KITURURU said...

Ulimbwende bonge la shughuli!:-(

Anonymous said...

Anony 01:34 na Simon, ha ha ha
Sicheki kwa furaha, ila habari hii imeniachia mbali kabisa, yaani mafuta kuondoa makunyanzi

Candy1 said...

Dah...yaani katika vitu vyote mtu anamfikiria binadamu mwenzie apate pesa...weird and absolutely disgusting

John Mwaipopo said...

kama yasinta ngonyani: tukiwaambia dunia ishaenda alijojo na pengine ishafika mwishoni, bado tu tamati yake mnabisha.

Born 2 Suffer said...

Kweli dunia inakwisha jamani binadamu hawana wema tena wamekua na roho mbaya, Wanasema dunia lakini sio hivyo walimwengu (binadamu ndio wabaya) hawana uaminifu tena, dunia ya sasa kila mmoja anafikiria pesa kitu cha mbele yupo tayari kumua binadamu mwenzake kwa ajili ya pesa.