Member of EVRS

Monday, 23 November 2009

Mungu yupo wapi?

Hivi Jumapili ni lazima uende kusali kanisani?

Mbona wanadai Mungu yupo kila mahali, sasa kwa nini uende kanisani?

Au huko kanisani ni mahali pa kuonyeshana mitindo ya mavazi, maana karibu kila mtu anakuwa nadhifu. Na ndipo Mungu humchagua mtu atakayepaa mbinguni siku yake ya kufa itakapowadia?!

Hiyo ndio changamoto niliyokutana nayo leo kwa mtoto wa miaka 10, aliyenikuta nimepumzika nyumbani, kwani hakuniona kwenye ibada ya leo.... anataka aelimishwe.

Nasema, jumapili njema, pia kama wewe ni muumini unayesali jumapili, jiulize huko kanisani unaenda au ulienda kufanya nini, isije kuwa mtoto alikuwa anasema ukweli. Maana kuna watu wanajikwatua........

2 comments:

Fadhy Mtanga said...

Si hao tu, wengine wanashindana kwa ufahari wa magari yao yalopaki nje ya kanisa. Lakini wengine....huwa mawindoni.

Simon Kitururu said...

Kanisani ni mbuga nzuri kweli kama mawindo ni watoto wa kilokole halafu kwao geti kali.:-(

Mtu hukawii kujiunga na kwaya wakati sauti kama chura!:-(