Member of EVRS

Tuesday, 3 November 2009

Kionjesho: Afya ya Macho Yako, Usalama wako

Madereva wa kwetu mara nyingi huwa wanapenda mteremko pale wanapotakiwa kupima macho yao kabla ya kupata leseni mpya ya kuendesha gari.

Sheria zinatakiwa waende kwenye hospitali za serikali waonwe na wataalamu wa macho (Bahati mbaya wataalamu waliopo huko mara nyingi ni wa ngazi ya chini).

Upimaji wa huko hufanyika kiushikaji, unatoa kitu kidogo unajaziwa fomu kwamba unaona mpaka kwa Mungu.
Niliwahi kumshuhudia dereva wa dala dala ambaye uwezo wake wa kuona mbali kwa uzuri ulikuwa ni meta nne (4) tu, hata kama ukimpa kupiga penati, basi hamuoni kipa.
Najua alikasirika sana nilipopiga panga form yake, lakini........

Hakuna anayezingatia usalama utakaofuatia kwa kumpa kibali mtu kipofu kuingia barabarani tena akiendesha gari la abiria....

Napenda kutoa vigezo vichache ambavyo vinapaswa kuzingatiwa
1. Uwezo mzuri wa kuona mbali kulingana na kipimo cha kuona mbali cha kimataifa
2. Uwigo wa kuona, yaani visual field inayokubalika kutokana na gari unaloendesha
3. Uwezo wa kuona rangi tofauti (colour vision), hasa rangi za kijani na nyekundu ambazo kuna baadhi ya watu wanazaliwa na kasoro ambapo rangi hizi hawazioni kabisa kama tunavyoziona sisi. Hii ni muhimu hasa katika zile taa za kuongoza madereva.

Hii ni kwa usalama wako wewe dereva na jamii inayokuzunguka. Kuna upofu unaoweza kuwa nao bila ya wewe kujijua, kwa nini usipimwe kwanza!!
Mambo ya chapchap katika maisha ya watu..... hatukosi kusikia ajali za kutisha...

Enjoy your day!

6 comments:

Halil Mnzava said...

Mzee ushauri wako ni mzuri sana ila kwa sisi wabongo hilo limeshindikana kwani mawazo yetu yanahisi kila kitu rahisi tu hata visivyo rahisi,matokeo yake tunaleta ajali bila sababu za msingi.
Tubadilike!!!!!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

OK ila kuna wanaoona vizuri zaidi kuliko vigezo hivyo, je wanapewa lesseni. au wana 'oversee'?

d'enricher said...

Hi Chip,

Thanks for droping by, and hello to you from malaysia.

Nice photos from your earlier posting

Simon Kitururu said...

Wanadai Bongo tambarare, mpaka leseni waweza ichukulia baa!:-(

Mzee wa Changamoto said...

Tatizo kubwa ni UBINAFSI. Mtu kujali na kulazimisha utakacho hata kama si halali. Kutaka kupata kila kitu kwa njia ya mkato na kwa bahati mbaya sasa imekuwa "kawaida kama sheria". Ukipinga unaonekana wa ajabu na sitoshangaa kama huyo dereva uliyempiga panga ukakutana naye wiki ijayo akichanja mbuga na basi la abiria na akiwa an cheti kinachoonesha kuwa anaweza kuwa dereva anayeona vema zaidi kuliko yeyote aliyepata kuishi ulimwenguni.
Hatujali UTU, hatuangalii athari, tunakwenda na "cha sasa"
Asante kwa tafakari nzuri Kaka
PamoJAH