Member of EVRS

Wednesday 25 November 2009

Historia ya Kutisha ya Bermuda Triangle


Kwa wale wanaopenda kujua matukio mbalimbali, basi watakuwa wanaifahamu vyema historia ya bermuda triangle.

Tangu mwaka 1945, zaidi ya meli 100 zimeshazama na vifo vya watu zaidi ya 1,000 vimeshatokea katika eneo hili ambalo ni maarufu sana kwa vyombo vya safari kupita. Pia ni eneo ambalo linasifika sana kwa kubadilika kwa hali ya hewa kwa haraka na bila kutarajiwa.

Matukio mengi yalitokea katika kipindi cha miaka ya 1940 - 1960, nayo yalihusu upoteaji wa kiajabu wa vyombo vya usafiri hasa ndege na meli.

Mwaka 1944, Dick Stern alikuwa anaruka na ndege ya kivita eneo hili, ghafla ilipoteza uelekea kwa muda na ikawa inaelekea kuanguka Bahari ya Atlantiki, lakin baadaye iliweza kutulia yeneyewe na kuendelea na safari vizuri. Na katika miaka ya 60 alipita tena eneo hilo akiwa na mkewe katika ndege ya kawaida wakapata msukosuko mkubwa.

Kwenye miaka ya 1945, 1958, 1964 na 1967 kuna ndege zilipotea tena katika eneo hilo ambapo mabaki yake hayakuweza kupatikana kabisa. Kuna baadhi ya marubani ambao waliwahi kuripoti kabla ya kupotea au kuokoka kwamba rada zao zilikupoteza uelekeo na kiasi kwamba wakashindwa kujua wako wapi, kuna mmoja aliripoti kuongezeka kwa kasi ya kwenda kwa ndege na kila kitu kikapoteza control, na baadaye vikarudi sawasawa.


Pia kuna rubani mmoja wa ndege ndogo alitaka kutua eneo hilo, lakini alipofika sehemu aliyotaka kutua, hakuiona ilhali watu waliokuwa chini walikuwa wanamuona na kumshangaa akizunguka tu hewani na kisha kuondoka. Baadaye alikiri kuzunguka juu baada ya kutokuona sehemu aliyotaka kutua wakati compass yake ilimuonyesha ameshafika.


Meli amabazo zimekumbwa na misuko sehemu hiyo zimekuwa zikiripotiwa kukutana na mvutano wa ajabu wa kwenda chini na mwishowe kuzama, au kukutana na machafuko ya bahari ya ghafla.

Kuna baadhi ya wafanyakazi wa meli walio okolewa waligeuka na kuwa vichaa!

Kituko cha funga dimba ni kile kilichoripotiwa mwaka 1967 kutoka kwa watu waliokuwa kwenye meli ya Elizabeth I pale waliposhuhudia ndege ndogo ikiwa mita chache kutoka walipo ikipotea ghafla ikiwa inaruka!!!!

Chungulia hapa usome zaidi


6 comments:

nyahbingi worrior. said...

nakusalimu mkuu.

Fadhy Mtanga said...

Mkuu nakushukuru sana kwa kunipa maarifa haya. Mimi huvutiwa sana na simulizi za eneo hilo.

twenty 4 seven said...

nakusalimu sana...

John Mwaipopo said...

sasa 'dereva' wa ndege ya president wetu anayajua hayo. si yuko huko jamaica. au jamaica iko mbali na pembetatu hii?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

pembe tatu hiyo

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kuna vipindi maalumu vya kitaalamu vilirushwa kuhusu eneo hili kutoka Discovery Channel na History Channel hapa Marekani. Wataalamu hawa walikuwa wanajaribu kutafuta hasa sababu inayosababisha meli na ndege kupotea katika eneo hilo. Kama unavyotegemea, wanasayansi huwa hawaendekezi mambo ya "kimiujiza" na nadharia ambayo walikuja nayo ni kwamba kuna mrundikano mkubwa wa gesi aina ya Methane katika eneo hilo. Gesi hiyo iko chini ya bahari na huwa inaripuka mara kwa mara. Walionyesha kwamba injini ya ndege ikiingiliwa na gesi hii kwa ghafla inaweza kuzimika na hivyo ndege kuanguka. Kwa upande wa meli walifanya jaribio na meli ilizama mara moja. Mpaka sasa nadharia ya wanasayansi hawa ni kwamba kuwepo kwa gesi ya Methane katika eneo hili pengine ndiyo kisababishi kikuu cha ajali nyingi - pamoja na sababu zingine za hali ya hewa.