Wapitiao njia hii mtaniwia radhi mkiona mambo hayaendi vyema.
Nimekuja kugundua unapoitwa kuwa msimamizi wa mitihani (external examiner) na kupewa jukumu la kutamka kwamba mtahiniwa huyu ameridhisha baraza la watahini na hivyo anastahili kufaulu mtihani ili asubiri graduation.. Ni adhabu kubwa.
Kwani inabidi na wewe urudi tena kwenye vitabu na kubukua ili mtahiniwa asije akakugonga nyundo ya kisogoni.
Kwa wiki mbili zijazo nitakuwa na kibarua cha kutoa maamuzi hayo. Mkiona blog imevaa suruali pwete, basi mjue vijana wamenitolea macho kweli kweli. Taabu lugha... kifaransa na kiingereza, lazima uvume kotekote ili wasikupige chenga.
Wikiendi njema
8 comments:
Kila la kheri kaka. Ni matumaini yangu mambo yatakwenda uzuri.
Nakutakia wikiend njema kaka Chib na kila kitu kitakuwa sawa
Naijua sana hiyo kazi. Usipokuwa makini unaweza kujikuta wewe ndiyo unafanya hiyo PhD badala ya mwanafunzi mwenyewe. Kasheshe inakuja pale mwanafunzi anapokuwa ametumia nadharia ambayo bado ni ngeni kwako. Inabidi uchepuke kweli ili usiachwe nyuma. Ndiyo maarifa yanavyosonga mbele.
Nenda ukatimize wajibu huo muhimu sana kitaaluma. Matunda yake daima huja na ridhiko linaloletwa na kujua kwamba umesaidia katika kueneza maarifa "mapya" hapa duniani. Kazi njema mkuu!
Lots of luck kaka! I hope you will be totally fine! God Bless! xx
amen!
kila la heri. kazi ngumu hiyo ati!
Jamani nawashukuru sana, nilikuwa nimezama kwenye buku japo nisiende kuwaaibisha wa-Bongo huku mitaani. Nipo fiti sasa, na wala sio kwamba nimeegesha, kwamba ukinitikisa basi nimebaki kama kikaragosi. Nimeshiba kabisa
Nahisi nimechelewa hapa!:-)
Ila nakuaminia Mkuu!
Post a Comment