Safari yangu ya Dar ilikuwa na matukio mengi ya kufurahisha.
Lakini penye mengi hapakosi na machache ya kuogofya.
Siku ya jumamosi nilikuwa nimetoka na familia kuelekea nje ya jiji kuona maendeleo ya hukoo kwa wananchi. Tukiwa kwenye high way ya kwenda Bagamoyo, kwa ghafla wife akashtukia jambo........, maana aliona mwenendo usio wa kawaida kwenye chini kidogo ya dashboard...
Alipo angalia kwa makini, hakukuwa na kosa, maana alimuona kiumbe wa malaika akitambaa taratibu kuelekea palipokuwa na gear ya gari, wakati huo mie nilikuwa nimekaza macho mbele maana mwendo kasi wa barabara hii, na uwingi wa magari, inabidi uende kwa uangalifu.
Kwa sauti ya staha na ukakamavu nikasikia mvumo wa sauti ukisema, Baba nanihii, nyoka huyo. Nilipiga jicho la haraka, na kweli alikuwa mwenyewe akielekea alikokaa waifu, ikabidi nitafute upenyo ili nisimame .. lakini nikaona anakuja kwangu hivyo nikamwambie amtwange, lakini... asilani akamkosa, na jamaa akabadili uelekeo wa kuja kwangu, na kugeuza uelekeo sijui alifikiri ndio salama huko.... Nilimtolea macho huku naelekea pembeni ya barabara, maana katikati ilikuwa ni hatari kwa magari mengine.
Niliposimama, nikaamuru watu wafungue milango waishie nje, lakini nyoka alikuwa mjanja sana, maana alishakimbilia sehemu ambayo waifu alikuwa ameweka miguu yake, na mlango ulipofunguliwa tu, yeye alikuwa wa kwanza kutoka na kutokomea porini!
Tulisimama hapo kwa dk 5 kupekua gari yote, maana watoto walikuwa usingizini kiti cha nyuma. Baadaye tuliondoka kuendelea na safari huku tukitweta.
Kwa sasa tunachukua tahadhari kupaki chini ya miti na kuacha madirisha wazi, maana hawa wageni nao jua likizidi, duh, lazima wajisalimishe.