Member of EVRS

Monday 28 November 2011

Ni siku ya Uchaguzi DR Congo na Egypt

Wapinzani wakidhibitiwa na askari wa Congo katika viunga vya jiji la Kinshasa

Leo ni siku ya uchaguzi wa rais na wabunge katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
Katika kampeni za kujinadi kwa wagombea, kulikuwa na matukio mengi ya uvunjifu wa amani ambapo polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wa vyama mbalimbali waliokuwa wanapingana. 
Katika kampeni, lugha mbalimbali zilitumika kama njia ya mawasiliano kutegemea na mahali kampeni za kisiasa zilipokuwa zikifanyaika. Lugha kuu zilizotumika zaidi katika kampeni hizo ni Kilingala, Kifaransa na Kiswahili.  
   
Huu utakuwa ni uchaguzi wa kwanza wa kipekee kwa muda mrefu, kwani gharama za uchaguzi huu zimegharimiwa na nchi ya Kongo yenyewe.


Askari wa Misri karibu na Tahrir square

Wakati huo huo, nchi ya Misri nayo leo inafanya uchaguzi wake wa kuwachagua wabunge wa mabunge mawili ya nchi hiyo.  
Itakumbukwa kwa wiki kadhaa sasa kulikuwa na maandamano ya kuipinga serikali ya Kijeshi inayotawala nchi ya Misri baada ya kiongozi wake wa siku nyingi, Hosni Mubarak kuachia madaraka kufuatia shinikizo la wananchi kumtaka kuondoka madarakani, ambapo alitii baada ya vurugu kubwa kuzidi nje ya uwezo wa utawala wake.  
  
Pia kwa Misri, uchaguzi huu unahesabika kuwa wa uhuru zaidi kwa miaka zaidi 30 iliyopita.
Kulikuwa na matukio ya ucheleweshaji wa makaratasi ya kupigia kura kwenye vituo kadhaa vya Cairo na Alexandria.  
  
Tunawaombea wamalize uchaguzi kwa amani ili waweze kizijenga nchi zao.

DRC Photo from The Telegraph
Egypt photo from Guardian

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

sijui niseme kila lakheri au? ok kila la kheri