Member of EVRS

Tuesday, 1 November 2011

Joseph Machele: Mtanzania Aliyepata Nishani ya Heshima ya Franklin Nchini Mexico

Joseph with assistant of the Ambassador to the US Embassy in Mexico city  Mr.  John Feeley Deputy Chief of Mission.caption

Joseph na Mkewe Mariana

Rafiki na wafanyakazi wenzake Joseph - Ubalozi wa Marekani Mexico
Joseph Machele, Mtanzania ambaye anaishi Mexico city nchini Mexico, amepata tuzo ya heshima ya Franklin (Franklin Award) ambayo hutolewa kila mwaka kwa wananchi wa Marekani au wanaofanya kazi katika idara za serikali ya Marekani ambao mchango wao kwa Taifa la Marekani katika fani mbalimbali za kazi zao umepita kipimo na kuweza kusababisha ufanisi mkubwa wa kazi au kuleta faida kwa uchumi au hali ya usalama kwa Marekani. 

   
Joseph Machele ambaye ni Mtanzania anayefanya kazi katika ubalozi wa Marekani nchini Mexico, ameweza kupata tuzo hiyo kwa utumishi bora na kuwa mbunifu. Allipata siku ya tarehe 12 Oktoba 2011, baada ya kupewa na naibu balozi wa Marekani nchini Mexico Bw. John Feeley.
Kupitia kujituma kwake na maarifa yake binafsi, aliweza kuokoa zaidi ya dola za kimarekani 115,000 kwa mwaka mmoja ambazo zingetumika kulipia gharama za kusafirisha samani na vifaa vya kukodisha na vitu vingine vidogo vidogo kwa ajili ya makazi ya watumishi wageni wanaoenda kufanya kazi kwenye ubalozi wa Marekani nchini Mexico.  
 
Mbali ya Joseph Machele kupata tuzo ya heshima, pia alijipatia kitita cha dola kama zawadi yake katika juhudi zake binafsi akiwa kazini. Alifanikiwa kuokoa kiasi hicho cha fedha kwa kuwashawishi wanaokodisha vifaa hivyo kutoa usafiri wa bure kusafirisha vifaa hivyo, jambo ambalo maafisa wa ubalozi wa Marekani walikuwa wanadhani ni kitu kisichowezekana kabisa. 
  
Hongera sana mdogo wangu Joseph kwa juhudi zako binafsi. Nakufahamu sana tangu kwenye ujana wako, ni mtu ambaye upo makini sana katika kazi zako. Usiishie hapo tu, bali ongeza bidii zaidi kwani mafanikio yako ni sifa kubwa kwetu sote tunaoishi Bara pevu na lenye utajiri mkubwa.

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hongera sana kaka Joseph

Anonymous said...

Hongera Joseph, wewe ni mkali, maana kupata ajira kwenye ubalozi wa hawa jamaa tena ukiwa ughaibuni si rahisi. Inaonekana una juhudi sana.

George, Uk said...

hongera sana Joseph, hii inaonyesha jinsi gani waTanzania tukiamua tunaweza, fikiri kuna kina joseph wangapi tanzania atuwatumii ipasavyo kukwamua taifa letu kiuchumi?
joseph wewe kaza buti,nakutakia kila la kheri.

Joe Machele said...

Asante sana ndugu zangu, hakika hii tuzo ni motisha tosha wa kuzidisha juhudi na maarifa kazini.

makumbi11 said...

hongera sana kaka yetu mpendwa, umetuonyesha njia bora wadogo zako ya kufwata, twakuombea Mungu akutangulie kwa kila jambo utakalolifanya

Subi said...

Pongezi sana Joe.
Hongera kwa uwakilishi mwema.