mchoro wa kuigiza wa chombo kinapolipuka moto mara kiingiapo katika anga ya Duni |
Awali walitegemea kingeanguka katika bahari ya Pacific, lakini katika hali isiyokuwa ya kutarajiwa, kilipoingia kwenye anga ya dunia (Earth atmosphere) kilionekana kama kimepunguza kasi ya kuanguka, hivyo badala ya kutarajiwa kuanguka siku ya ijumaa, NASA ilikadiria kitaanguka jumamosi usiku au jumapili alfajiri.
Chombo hicho chenye ukubwa kama wa basi kubwa, na kinachokadiriwa kuwa na uzito wa tani 6, mpaka sasa hakijulikani kilipo, na wala hakuna mtu aliyekwisha kutoa taarifa kama wameona mabaki yake. Na kwa kuwa mpaka sasa hivi NASA haijapokea taarifa yoyote ya majeruhi au madhara ya aina yoyote, wanaamini chombo hiki kimeanguka baharini, lakini hawajui ni sehemu gani.
Bado wantafuta habari ya wapi mabaki ya chombo hiki yataonekana ili wawe na uhakika ya kuwa ni kweli kimekwisha anguka kwenye uso wa dunia.
Pata habari zaidi hapa