Member of EVRS

Thursday 7 April 2011

Rwanda Leo Yaadhimisha Miaka 17 ya Mauaji ya Kimbari Dhidi ya Watutsi

Leo imetimia miaka 17 tangu mauaji ya Kimbari ya Rwanda kutokea.
Kwa miaka yote tangu mauaji hayo ya kikatili dhidi ya Watutsi yafanyike, tarehe kama ya leo watu hukumbuka matukio ya mwaka 1994 kwa hotuba na baadhi ya watu kutoa ushuhuda wa matukio ya wakati huo. Kwa ujumla huamsha hisia na uchungu kwa manusura, baadhi yao hupata mfadhaiko wa akili kiasi cha baadhi yao kulazimika kupelekwa hospitali kwa matibabu. 
  
Katika hotuba ya kitaifa siku ya leo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, katika machache aliyozungumza, hakuficha hisia zake na hasira kwa wale wanaoendelea kupinga mauaji hayo ya kimbari dhidi ya watutsi (Genocide against Tutsis), na pia aliyashutumu mataifa yanayoendelea kuwaficha watuhumiwa wakuu wa mauaji hayo ambao wamejificha katika baadhi ya nchi hususan za Ulaya, na kukataa kata kata kuwatoa kwa ajili ya kushitakiwa kisheria. Alitoa hisia yake ya kuwa nchi hizo zinaogopa kuwatoa kwa sababu zinaogopa ushahidi utakaotolewa na hao watuhumiwa, utadhihirisha ni jinsi gani nchi hizo zilishiriki katika kufanikisha mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi wa Rwanda.  
  
Siku kama ya leo huwa ni mapumziko ya kitaifa, na shughuli zote za kikazi husimamishwa ikiwa ni pamoja na maduka kufungwa na shughuli zote za kibiashara kusimamishwa.  
 
Jinsi nilivyoiona siku ya leo, sikuona tofauti na siku nyingine za maadhimisho ya mauaji hayo hasa nikilinganisha na maadhimisho ya miaka iliyopita, kwani jiji la Kigali limepooza sana, na watu wachache wanaotembea barabarani, sura zao zinaonyesha huzuni kubwa.

Nakubaliana na msemo wao NEVER, NEVER... IT WILL NEVER HAPPEN..... NEVER AGAIN

4 comments:

EDNA said...

Mungu azilaze roho za marehemu wote mahala pema peponi Aamina.

Anya said...

Hi Chib

I hope it wil NEVER happens again!!!
So so sad lines today ...

Simon Kitururu said...

NEVER AGAIN ! Sounds good but...
Does HISTORY really teaches PEOPLE anything,....
... putting all that history that SEEMS TO keep repeating itself in the world into consideration?:-(

emu-three said...

Historia ina mafunzo mengi, lakini watu kama bin-adamu tulivyo ni wepesi wa kuasahau, natumaii hilo lilitokea na tujifunze nalo, ...kwani kwa hali ya kawaida unajiuliza `kwanini umchukia mwanandamu mwenzako kiasi hicho,...na kwanini tuchukiane wakati sisi na watoto wa baba mmoja na mama mmoja, Adam na Hawa...