Member of EVRS

Friday 15 April 2011

Muswada wa Marejeo ya Katiba ya Tanzania 2011 Waondolewa Bungeni

Kamati ya Bunge inayohusiana na masuala ya uundwaji wa sheria, imetoa mapendekezo ya kuongeza muda wa kupitia muswada wa sheria utakaohusu mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Sababu kubwa ni:
  • Kutoa muda zaidi wa kamati hiyo kupitia muswada huo
  • Kufanyia kazi mambo ambayo yameonyesha kuleta utata
  • Kuwapa muda zaidi wanachi wa Tanzania kutoa maoni zaidi
  • Kuandaa muswada kwa lugha ya kiswahili ili watu wauelewe zaidi kuliko kutafsiriwa na watu wachache
 
Spika Anne Makinda ameridhia, lakini ametoa tahadhari ya kuwa muswada huo haumilikiwa na chama chochote cha siasa, pia amewaasa watu wote kuupitia taratibu bila jazba wala kuleta fujo. Mwisho aliiagiza kamati kumpa ratiba ya shughuli za kurejea muswada huo, na kueleza lini watakuwa tayari kutoa muswada huo tena kwa lugha zote za kiswahili na kiingereza.
    
Hapo awali, muswada huu ulileta fadhaa na ghadhabu kwa baadhi ya watu wakiupinga kwani ulikuwa umekataza baadhi ya mambo kujadiliwa katika maoni ya marekebisho mapya yatakayopendekezwa.

2 comments:

emu-three said...

Katiba ni kitu nyeti kwakweli, na ni vyema jamii, makundi ya watu na hata ikibidi kila mtu akahusika na hiyo katiba, hii itaondoa manung'uniko, kwani katiba hii iliyopo iliundwa kwasababu maalumu, na ilikuwa iwe hivyo, kwa muda huo, sasa yapo mabadiliko mengi, na hina haja ya kufichana tena.

Upepo Mwanana said...

Uamuzi mzuri na wenye manufaa. Naona wameanza kubadilika