Member of EVRS

Tuesday 8 February 2011

Sababu ya Adimiko Langu

Yote ni maisha.

Kwa kipindi fulani nilikuwa nimeshindwa kuparaza blogu hii kwani nilifikwa na mkasa kidogo, wahenga wanasema ajali haina kinga.

Nilikuwa nimelazwa hospitalini kwa mara ya kwanza japo kwa siku moja baada ya kukumbwa na ajali. Kwa sasa nimesharuhusiwa na nipo nauguza vilivyobakia bakia nyumbani.

Tutaonana pindi nitakapokuwa na nafasi, kwani nimeshauriwa na daktari ati nipumzike,sijaelewa kama kublogu ni kazi au ni ruksa kama nimeambiwa kupumzika.

Yote kwa yote, leo niliguswa sana na mjadala wa bunge nikiwa siamini kuona wapinzani wakitetana kama vile ni maadui wakubwa!

Kila la heri kwenu nyote!

11 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Pole sana kaka na yalikupata. Mungu mkubwa, na shkrani kwa kutuhabarisha na sasa hofu zimepungua si unajua sisi sote ni ndugu.

chib said...

Ahsante Da Yasinta

Simon Kitururu said...

Ugua pole Mkuu! Na pole sana ! Ila ulipata ajali gani tena Mkuu!?

chib said...

Thx Kitururu, ngumu kusema vyote,lakini ilitokea kwa bahati mbaya lakini nilipata jeraha la kichwa na fahamu nikawagawia jamaa lakini wakanirudishia baada ya muda mfupi. Najaribu kusahau ili nipate nafuu haraka

EDNA said...

Duuuh pole sana kaka!GET WELL SOON.

Unknown said...

Kila jambo lina wakati wake.

KUNA WAKATI WA KUCHEKA NA WAKATI WA KULIA, KUNA WAKATI WA KULIMA NA WAKATI WA KUVUNA. KUNA WAKATI WA KUFANYA KAZI NA WAKATI WA KUPUMZIKA.

Kuna wakati ambao kila Jambo lina wakati wake kana ilivyo sasa kwako.

Huo ndio wakati ulionao...na MUNGU naye yupo nawe.

Tunakuombea jipe hakika ya kupona.

UMESHAPONA BWANA.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kweli mganga hajigangi, nani kakulaza wakati kazi yako ni kuwalaza wengine??

Anya said...

I cannot read this
but its always sweet to visit and look at you fish :-)
I have feed all ....
LOL
Enjoy your weekend !!

Kareltje =^.^= Betsie >^.^<

¸.•´¸.•*´¨) ¸.•*´¨)
(¸.•´ (¸.•´Anya

Goodman Manyanya Phiri said...

Pole!

Simon Kitururu said...

Nimatumaini yangu unaendelea vyema Mkuu!

chib said...

@ Simon, naendelea muswano, nimerudi kazini tangu jana.
Shukrani wanachama wenzangu katika dunia hii ya kublogu