Member of EVRS

Thursday, 17 February 2011

Mlipuko wa Mabomu Tanzania: Tunajifunza nini?

Wahanga wa mabomu ya Gongo la Mboto wakigaa gaa na maumivu huku wakiendelea na kupata huduma sakafuni katika hospitali zetu

Usiku wa kuamkia leo, viunga vya Gongo la Mboto kulikuwa na balaa la aina yake mara baada ya mabomu kulipuka kutoka kwenye maghala ya Kikosi cha jeshi la Wananchi wa Tanzania huko huko Gongo la Mboto.

Maghala yote ya kuhifadhia mabomu yanasemekana yameangamia kabisa ikiwa ni pamoja na mabweni mawili ya askari, magari na nyumba kadhaa za wananchi walikuwa wanaishi jirani na eneo la kikosi hicho.

Wanajeshi waliokuwa kwenye mabweni, inasemekana wamesalimika baada ya kukimbia mara milipuko ilipoanza.
Chanzo hakijajulikana, na huenda kisijulikane kutokana na mazoea ya kutotangaza taarifa za ukweli. 
 
Wakazi wa maeneo ya tukio walipagawa kutokana na milipuko iliyoanza kwenye muda waasaa 2 usiku mpaka alfajiri, na milio hii ilisikika karibu maeneo yote ya Dar es Salaam.

Taarifa mbalimbali zinasema watu wengi wanahofiwa kufariki, na tayari idadi inayozidi 25 wamekwishatambuliwa kufariki. na mamia kadhaa kujeruhiwa. 
  
Kutokana na mtawanyiko wa watu, wengine walijikuta wametoka mbio kutoka Gongo la Mboto hadi Msasani bila kujijua, ni bahari tu ndio iliyowashitua kuwa wamefika ng'ambo ya jiji na hawawezi kuogelea kukimbia zaidi. Pia kuna watu walijikuta wamekimbilia kwenye miji mingine na kusahau sehemu ambazo jamaa zao wanaishi.

Cha kushangaza zaidi ni pale baadhi ya mbwa walipokutwa nao wamekimbilia chini ya uvungu wa vitanda vyumbani mwa watu (Hii imethibitishwa) labda kwa kuogopa kelele za milipuko au kusalimisha maisha yao. 
  
Sijajua kama kuna haja ya kuipa ushauri serikali kuhusiana na uhifadhi wa mabomu au wamekwisha pata funzo kwa sasa hasa ukizingatia tukio lingine la mabomu yale yaliyolipuka Mbagala miezi kadhaa iliyopita.

Picha hiyo hapo juu nimeihamisha kutoka kwenye mtandao wa Michuzi.
Pata picha zaidi kutoka kwa Michuzi

5 comments:

SIMON KITURURU said...

Stori hii mie mpaka nashindwa pakuanzia!:-(

Teuvo Vehkalahti said...

Greetings from Finland. This blog is fun to explore, through other countries, people, culture and nature. Come take a look Teuvo pictures blog. And tell all your friend, why you should visit Teuvo pictures blog. Therefore, to obtain your country's flag rise higher Teuvo blog pictures of the flag collection, Happy Thanksgiving to Teuvo Vehkalahti Finland

Anya said...

Sounds very dramatic !!!
That picture looks very sad :(Hugs

Kareltje =^.^= Betsie >^.^<

¸.•´¸.•*´¨) ¸.•*´¨)
(¸.•´ (¸.•´Anya

Trevor Woodford said...

Very interesting post -full of the drama..!

chib said...

Anya and Trevor... That was a really bad story, it happened when amunition store close to civilian residency erupted at night destroying more than 20 armouries, several houses, cars and other properties. Hundreds of people injuried and several deaths!
You can get google poor google swahili translator to get some of my posts