Member of EVRS

Monday 28 February 2011

Maudhi ya TBC1 Usiku wa Manane!


Shirika la Utangazaji la Tanzania, kupitia kituo chake cha TBC 1 jana usiku lilizidiwa na maarifa ya teknolojia pale kiliposhindwa kuoanisha picha na sauti kwenye kipindi kilichokuwa kinarushwa muda wa saa 7 za usiku wa kuamkia leo kwa saa za nchi za Afrika mashariki. 

Nilikumbana na tatizo hilo wakati nilipokuwa nimetoka kazini usiku kwa saa za sehemu nilipo ilikuwa bado ni mapema kidogo kuliko Tanzania. Wakati TBC 1 ikiwa inarusha matangazo ya kituo cha televisheni cha Urusi (RT) ambacho kilikuwa na matangazo yanayohusiana na utafiti wa kisayansi kwa kutumia panya maalumu.  
  
Badala ya kusikika sauti za matangazo yaliyokuwa yanatangazwa, kulisikika milio ya muziki wa taarabu, tena huenda nyimbo hizo zikawa ni zile za kwenye harusi. Kwa ufupi, ilikuwa ni kero kwa sisi tuliokuwa tunataka kusikiliza maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani. ilichukua kama nusu saa kukiwa na tatizo hili, na baadaye TBC 1 maji yaliwazidi kimo, wakaamua kuondoa sauti kabisa kwenye matangazo ya muda huo, na kubakiza picha pekee. Hapo ilitubidi tuendeleena kuangalia TV "bubu", hadi ilipofika saa 8.00 za usiku (EAT) nikaamua kulala kwa kuona ya kuwa nilikuwa napoteza muda tu.

Nilimkumbuka Tido Mhando ambaye aliacha au kuachishwa kazi TBC kwa madai ya kuwa mkataba wake ulikuwa umekwishamalizika huku kukiwa na fununu zilizokuwa zimezagaa ya kuwa aliwaudhi watu fulani wakati wa kampeni za uchaguzi wa oktoba 2010 na hivyo kuamua kutoongeza mkataba wake kwenye shirika la TBC.

Bado najipa moyo ya kuwa hilo lilikuwa ni tatizo la bahati mbaya, japo inashangaza kuona mafundi wa mitambo (IT) wa TBC walishindwa kurekebisha tatizo hili kwa zaidi ya saa moja, na kuachia taarabu ikiunguruma kwa zaidi ya nusu saa.

Mwendo mlima!

1 comment:

Anya said...

translater don't work :(

I try it later again !!