Member of EVRS

Sunday, 27 February 2011

Makazi ya Rais Joseph Kabila Yashambuliwa

Watu ambao bado hawajajulikana au ambao imeamuliwa wasitajwe majina yao leo hii wameshambulia makazi ya rais wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bwana Joseph Kabila katika eneo la Gombe jijini Kinshasa, ambako katika eneo hilo kuna ofisi nyingi za balozi za nchi mbalimbali.
Walinzi wa makazi hayo walikuwa makini na kufanikiwa kuwaua washambulizi hao kwa jumla ya 6 papo hapo na wengine kukamatwa.

Inasemekana kwa uchache, watu tisa wamekwishapoteza maisha. Habari ambazo bado zimetoka punde, zinadai waliokuwa wameshambulia makazi hayo ni makomandoo, na walikuwa na silaha kubwa za moto. Inadaiwa wakati wa shambulizi hilo, Rais Kabila alikuwepo kwenye makazi yake, ingawa kuna taarifa nyingine zinadai hakuwapo muda huo, ila alirejea baada ya kusikia kuna tukio katika makazi yake.

Mara baada ya milio ya risasi kusikika, watu waliokuwa karibu na makazi ya rais Kabila walitawanyika kwa mbio kali sana.

Kwa sasa barabara zote karibu na Makazi ya Kabila zimedhibitiwa kwa askari na vifaru vikiwa vimeziba njia zote za kuelekea makazi hayo ya Rais.

Rais Joseph Kabila anatarajiwa kumaliza muhula wake wa urais baadaye mwaka huu, na kutakuwa na uchaguzi mwingine hapo Novemba mwaka huu.

2 comments:

Anya said...

Hi Chib

It sound very dangerous !!!
:(

Have a restfull and peaceful Night
Gr. Anya

chib said...

Hi Anya, it is scarring especially for us neighbours!
Have a goog night too