Member of EVRS

Thursday 2 December 2010

Tanesco Yaanzisha Blogu


Kwa wale wanaotaka kujua ratiba za mgao wa umeme, kutoa maoni kuhusu namna ya kuijenga na kuimarisha Tanesco na kadhalika, basi habari nzuri ni kuwa Tanesco wameanzisha baraza la mawasiliano wakitegemea msaada mkubwa kutoka kwenu wananchi mnaoishi Tanzania ili muwasaidie waendelee kuwaangazia maisha

Wanatoa rai ya kuwasaidia na sio kuwatukana kwani matusi si ustaarabu.

Nimeiona kwa Subi na pia link yao ni hii hapa

4 comments:

Fadhy Mtanga said...

alhamdullillah.....nashukuru sana kwa kutujuza jambo hili....kilichobaki sasa ni kuhamia huko kwenye blog tuone kwanza wanasema nini

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Miaka na miaka nilizoea kuona visanduku vya maoni katika milango ya kuingilia katika ofisi nyingi za serikali. Naamini kwamba wananchi walikuwa wanatumbukiza vikaratasi vyenye maoni yao humo - pengine wakilalamika kuhusu rushwa, uzembe, uonevu na hata kusifia pale walipofanyiwa mema.

Je, kuna mtu aliyekuwa anatilia maanani na kufanyia kazi maoni ya wananchi hawa? Kama jibu ni ndiyo mbona hakukuwa na mabadiliko yo yote kuhusu kero kama rushwa na uzembe katika sehemu za kazi?

Sioni jipya hapa. Kama mfumo umeoza basi hakuna cho chote kitakachobadilika. Watu watatoa maoni na mapendekezo weeeeee lakini bila kubadili mfumo hakuna kitakachobadilika. Nadhani ambacho kila Mtanzania anataka kusikia ni lini Tanesco itaweza kuwa na uwezo wa kutoa umeme wa kuaminikia kwa siku 365 kwa mwaka na siyo vinginevyo. Angepatikana mshindani katika sekta hii ya umeme pengine nayo ingesaidia na kuwaamisha hawa Tanesco.

Ngoja tuone kama hii blogu itasaidia chochote!

Simon Kitururu said...

SIna uhakika na hili ingawa najitahidi kweli kuwa chanya aka OPTIMISTIC!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

duhu! heri mimi naishi Bukoba!