Wanyarwanda jana usiku wamekesha kwenye uwanja wa Taifa - Amahoro wakipokea matokeo kutoka sehemu mbalimbali ya kura za rais.
Naweza kusema kuwa karibu wote waliokuwepo kiwanjani walikuwa wapenzi wa RPF ambacho ndio chama cha Rais wa sasa Paul Kagame. Uwanja ulikuwa umejaa na kutapika kwa idadi ya watu.
Shughuli hiyo ya kupokea matokeo moja moja, ilikuwa inaonyeshwa na Televisheni ya Rwanda, na uwanjani watu walikuwa wanashuhudia kwenye screen kubwa na kushangilia vilivyo.
Sherehe hizo maarufu kama "Hakuna Kulala" ziliendelea kuanzia saa 12 jioni hadi asubuhi. Rais Kagame naye pia alihudhuria sherehe hizo.
Matokeo rasmi bado hayajatangazwa na tume ya uchaguzi, kwani bado inaendelea kupokea matokeo. Mwelekeo unaonekana Kagame atashinda kwa zaidi ya asilimia 95.
Leo nikiwa tayari kwenda kazini, kabla sijatoka, nimetaarifiwa kuwa leo ni siku ya mapumziko. Sijajua ni mapumziko ya kusheherekea ushindi, au watu wamechoka kwa kukesha usiku mzima wakishangilia au........ duh!
Imenibidi nitundike madaluga, nikikusanya nguvu, kwani kesho nitakuwa na kibarua mara 3 zaidi ya siku zote, kwani kazi za siku 2 zimelala, ukiongeza na kesho.. lah, laiti ningejua mapema ...........
3 comments:
Asante sana Doc Chib kwa updates. Nafurahi kusoma kutoka 'jikoni'.
Hongera kwa siku ya mapumziko ya kustukiza na pole in advance kwa ajili ya kesho.
hahaha!ungejua mapema ungefanyaje Chib?hahaha ungekuja tz chap?au ungekesha nao?thanks for these news, hivi ni kutoka mioyoni wanyarwanda wanampenda kagame?na wanaompinga wanampinga toka moyoni au ni uchu wa madaraka?au ni kutoa changamoto tu?au ni mamluki?waliotumwa na Kagame ili kuonesha kuna vyama vingi ila kiukweli ni walewale?kuna mengi siyaelewi naona nipo gizani plz Chib naomba unieleweshe.
Johnson Minja
Johnson, mie kinachoniudhi hapa, ni mapumziko ya kushtukiza yaani mtu anapojisikia. Saa nyingine utajkuta tumeenda mpaka ofisini, na kuelezwa ati asubuhi hiyo wametangaza mapumziko, saa nyingine watu wanadamka mapema na kupeleka watoto shule, wakifika, geti limefungwa, ati sikukuu imetangazwa siku hiyo, wakati mwingine tunakuwa tumechoka na kutaka kulala zaidi, sasa.... upo hapooo
Post a Comment