Rais wa Marekani, Barack Obama, ameshinda tuzo ya amani na Nobel 2009 baada ya kushika madaraka ya urais kwa miezi 9 tu!
Kuchaguliwa kwake kumekuja kwa mshangao wa wengi na bla kutarajiwa, kwani watu wengi hawakuwa wamemfikiria, na katika majina yaliyokuwa yanatajwa hapo awali, yeye hakuwemo. Mpaka sasa haijajulikana ni nani aliyempendekeza.
Pia ni kiongozi wa kipekee ambaye amepewa tuzo hiyo kwa juhudi za amani, hata kabla matunda ya juhudi zake hayajaonekana hasa huko mashariki ya kati.
Wasemaji wanasema hili ni pigo jingine kwa utawala wa rais aliyemtangulia George Walker Bush ambaye utawala wake ulichukuliwa kuwa wa mabavu kwa nchi za mashariki ya kati.
Binafsi, nampongeza rais Obama kwa mafanikio na ushindi huo.
5 comments:
hii inatosha kwa mimi kwa sasa kusema duh!
nahisi hili jamaa lichawi!
Nami pia nampongoza sana Hongera Barack Obama.
John...., yaani, umenifanya nifurahi weekend hii yote. Sijui niseme huyu jamaa ana kismet au vp!!
Nyota yake ni angavu
Post a Comment