Member of EVRS

Sunday 18 October 2009

Mafua ya Nguruwe - Rwanda

Wiki iliyopita nilitoa taarifa ya ugonjwa wa mafua ya nguruwe kuingia hapa Rwanda baada ya kumpata waziri wa serikali.

Hali ilikuwa ya kuogofya kwa watu wengi, hasa ilipogundulika ya kuwa kuna watu 12 wamekwisha ambukizwa kwa muda mfupi sana ikiwemo na watoto wa waziri mwenyewe.
Mpaka sasa hakuna kifo kilichotokea na wagonjwa wote wanaendeelea vizuri.

Mwanzoni mwa wiki hii. Mkuu wa idara ya watoto katika hospitali alipolazwa mtoto wa waziri huyo aliyeleta mafua hayo Rwanda kwa siku 2 na kuruhisiwa baada ya kuendelea vizuri, alifukuzwa kazi wakisema idara yake ilifanya uzembe kwa kushindwa kugundua ugonjwa huo mapema. Hakupewa nafasi hata ya kujieleza na kitendo hicho kiliwaudhi wafanyakazi wenzake.

Hata hivyo, waziri wa afya ameingilia kati suala hilo na kuliangalia upya kwani inaonekana hatua iliyochukuliwa ilikiuka ngazi mbalimbali.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nashukuru kama hakujatokea kifa. Hata sisi hapa umefika na mtu mmoja amekufa.

John Mwaipopo said...

Mafua ya nguruwe yananipa ahueni kwa kitu kimoja tu; hayahusiani na masikini na mafukara. ona sasa kumbe ni mtoto wa kigogo ndo kaenda huko na kuyazoa ya kuyazoa na kuleta rwanda. nina wasiwasi pia aliowaambukiza sio pangu pakavu tia mchuzi.

hilo la kufukuzwa kazi huyo mtu namuachia ngoswe. kubeba mifua waibebe wenyewe huko kwenye picnic zao ulaya, kazi afukuzwe mwingine. kweli inzi hata aruke vipi hawezzi kuwa ndege asilani

chib said...

Sikueleweka vizuri, aliyeleta mafua hayo ni waziri mwenyewe, na watu aliowaambukiza wa kwanza walikuwa ni watoto wake mwenyewe. Baadaye watu wengine waliambukizwa kutoka kwa watoto wake. Kuna shule zimefungwa kwa sasa