Member of EVRS

Friday, 10 July 2009

Upandikizaji wa Moyo katika Binadamu




Je unajua ya kuwa duniani kuna watu zaidi ya 800,000 ambao wamepimwa na kuthibitishwa ya kuwa mioyo yao ina matatizo ambayo hayatibiki kwa njia yoyote zaidi ya upasuaji wa kubadilishiwa mioyo hiyo na kuwekewa mingine (heart transplant). Hii ni mbali na wale ambao wako kwenye nchi ambazo hazina vipimo vya kutosha.


Na pia, kwa mwaka kuna wagonjwa 3,500 tu ndio hufanikiwa kufanyiwa upasuaji huo ulimwenguni kote ambapo moyo mpya huchukuliwa kwa mtu aliyekufa (allograft) na kuacha wosia kwamba viungo vyake vitumike kuwasaidia watakaohitaji, na ambao inasemekana unafanya kazi vizuri kwa takribani miaka 15. Kwa mioyo mingine itokayo kwa viumbe wengine (xenograft) na ya bandia, imekuwa haina mafanikio sana na hulazimika kutolewa na kuwekewa mwingine mapema zaidi.


Upasuaji wa kwanza wa kubadilisha moyo ulifanyika USA tarehe 23 jan 1964 wakati moyo wa sokwe ulipowekwa kwa mtu ambao ulidumu kwa dakika 90 tu, na ile ya kupandikizwa kwa moyo wa binadamu ilifanyika Afrika kusini tarehe 3 Dec 1967, na mgonjwa aliishi kwa siku 18 kabla ya kufariki kwa homa ya mapafu.
Ujumbe wangu kwako: Moyo hautengenezwi kiwandani. Tuwe tayari kujitolea mioyo yetu pindi tukikata kamba ili ambao wanahitaji waweze kupewa na kendelea kuishi!

4 comments:

Fadhy Mtanga said...

Ahsante kaka Chib kwa changamoto hiyo. Nikifa moyo wangu wa nini tena. Kama inawezekana, bora usaidie wengine.

chib said...

Fadhy, naona tupo pamoja. Ahsante kwa mchango wako

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli hata mimi nipo pamoja, yaani kusaidia wengine.

Egidio Ndabagoye said...

Ina maana Familia ya Michael Jackson imeshindwa kununua moyo mfalme wa pop aendelee kuishi?