Member of EVRS

Monday 20 July 2009

Dhana ya majinni na Mizuka




Leo nimeamua kumwaga habari ambayo watu wengi huwa wanaiogopa.

Nimepata changamoto ya kuandika habari hii hasa baada ya kuwauliza wafanyakazi wenzangu uwepo wa kiatu kimoja cha mwanamama kwa muda mrefu, nafikiri tangu nimekuja hapa Rwanda hicho kiatu nilikukuta katika chumba ambacho tunakitumia kwa uchunguzi katika kazi yetu.

Hakuna anayejua ni cha nani, na inaonekana hakuna hata mtu mmoja ambaye kama alikichukulia umaanani.
Mmoja alizungumza kama utani ya kuwa ..labda ni cha mzuka hicho....., tukacheka wote na kuendelea na kazi.

Nikatafakari sana na wakati wa mapumziko ya chakula cha mchana nikaamua kusaka habari za mizuka, mashetani na majinni katika mtandao.

Baada ya kusoma hapa na pale, nachoweza kusema ni kuwa habari za majini ni mkanganyiko tu, wapo wanaodai ni viumbe walioumbwa kama kioo (transparent), wengine wanadai wana ngozi laini kiasi kuwa hawezi kuonekana, wengine wanadai wapo wa aina 3 ati wapo wanaopaa na wako kama upepo tu, wengine wanakuja kwa mfumo wa wadudu wataambao kama majoka, nge nk na wengine wana maumbo yasioelezeka na wanaweza kutokea na kupotea.

Pia wanadai huwa yana uwezo wa kuzaana na pia kufa!

Pia wanadai huwa wana majina mbali mbali katika lugha ya kiarabu tutataja baadhi yake:

( a ) Jinni : Anapokusudiwa jinni tu. Na maana ya neno jinni ni kitu kisichoonekana au kilichofichika.
( b ) Aamir : Anapokusudiwa yule anaishi katika majumba ya watu.
( c ) Shetani : Anapokuwa na shari
( d ) Rauhaan : Yule anaewatokezea watoto
( e ) Afriit : Anapokuwa na nguvu za kupindukia

Habari iliyoniacha hoi kabisa, ni pale waliposema ya kuwa huwa yanatembea yamevaa kiatu kimoja tu!!

Ukipenda kusoma habari ya kufikirika, bofya hapa

5 comments:

Anonymous said...

Majuzi umetuletea li-paka la ajabu, leo tena mizuka. Habari ninzuri, lakini usiku unaweza kuota

Anonymous said...

It seems you are in love with these scary stories. Are you a believer of of these things?

Yasinta Ngonyani said...

menikumbusha nilipokuwa mdogo nimewahi kuona watu wanaangua chini na kuanza kucheza huku wakipigiwa ngoma kwa sababu ana majini. Na baada ya muda anakuwa kama kawaida eti yale majini yanakuwa yametoka. Na yule mtu anakuwa kachoka kama amefanya kazi nzito kweli. Lakini sina uhakika kama kuna majini.

Simon Kitururu said...

DuH!

Na wasiwasi labda na majini yashaanzisha blogu fulani tuzitembeleazo siye bila kujua:-)

chib said...

Kitururu, you made my day :-)

Hey Anony 11.08 I always like to watch movies or reading stories which make my hair stand on end. I also like to ask myself for anything which seems to be abnormal, and also I like to cast out fear of uncertainity.

Nitakuja na mada murua ya viini macho, ndipo utagundua kuwa mambo yote tunayoyaona mengine ni mawasiliano tu kati ya ubongo na macho ndio huchelewa, na hivyo tunaona visivyokuwepo