Wiki iliyopita nilitoa makala kuhusiana na upandikizaji wa moyo, na wiki hii nimepata habari ya mtu aliyeokolewa maisha yake kwa kupandikizwa moyo.
Pichani juu ni Hanna Clark ambaye ana miaka 16 sasa, binti huyu alipandikizwa moyo sambamba na moyo wake wa asili mwaka 1995 baada ya kuonekana moyo wake ulikuwa hauwezi kufanya kazi sawasawa hapo mwaka 1994, wakati huo akiwa na umri wa miezi 8 tu.
Siku zote amekuwa akiishi na mioyo miwili inayofanya kazi pamoja huku uliopandikizwa ukiwa ndani ya moyo wake wa asili uliokuwa umechoka.
Kutokana na madawa aliyokuwa anapewa kupunguza kinga ya mwili ili moyo aliowekewa usidhurike alipata saratani ambapo madaktari walilazimika kupunguza dawa zake ili saratani isisambae, na baadaye moyo aliowekewa ulianza kushambuliwa na mwili na kuanza kuharibika, lakini cha ajabu ule moyo wake wa asili ulikuja kugundulika kuwa ulikuwa umepona wenyewe na kuwa ulikuwa unafanya kazi vizuri kabisa na hata madaktari wake hawakutegemea.
Kwa sasa binti huyu anafanya shughuli zake kama kawaida ikiwa na baadhi ya mazoezi, na huku akiendelea na matibabu ya saratani
Najaribu kutafakari maendeleo ya sayansi katika fani ya tiba, kama angekuwa mitaa ya kwetu huku, labda watu wangekuwa wanakaribia kufanya kumbukumbu ya kifo chake miaka 16 iliyopita.
Tunahitaji kuwa wachangiaji wa viungo, kuna siku wajukuu zetu wataokolewa!!
2 comments:
Hii kweli ni Miracle
Ahsante sana kwa kushare nasi miujiza hii. Tunajifunza mambo mengi. Nadhani kubwa ni UPENDO. Ukiwa na upendo unakuwa radhi kutoa viungo vyako pindi viza yako ulimwenguni itakapo eksipaya.
Ni hayo tu.!
Post a Comment