Member of EVRS

Saturday 11 December 2010

Tanzania Bara Yaingia Fainali ya CECAFA Tusker Challenge Cup 2010

Timu ya mpira wa miguu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) hapo juu wakishangilia ushindi, jana ilifanikiwa kuingia fainali ya kombe la CECAFA baada ya kuwafunga timu ya Uganda (The Cranes) kwa mikwaju ya penati 5 - 4


Kipa namba moja wa Kilimanjaro Stars, Juma Kaseja kama anavyoonekana hapo juu akiiokoa penati moja ya waganda na hivyo kuifanya Tanzania Bara kuingia fainali.

Fainali itakuwa kesho, ambapo Tanzania Bara itapambana na timu ya Ivory Coast. Hata hivyo ni lazima kombe libaki Tanzania hata kama Ivory Coast itashinda, kwani timu hii ya Afrika Magharibi ilialikwa tu kupasha moto mashindano, na sheria za CECAFA timu mualikwa huwa haipewi kikombe, isipokuwa inapewa zawadi iliyopangwa kwa mshindi wa kwanza, na kikombe huchukuliwa na nchi mwanachama aliyeshika nafasi ya juu.

Kwa maana hiyo, Kilimanjaro Stars ndiyo itakayopewa kombe hilo kwa matokeo ya aina yoyote.

Tuna imani Tanzania Bara itashinda na kuchukua kombe hilo.

Picha kutoka kwa michuzi

1 comment:

emu-three said...

Na kombe tumelichukua kwa bao moja...afadhali, lakini jina litatufanya tusipande chati..`Kilimanjaro Star...mmmh, sijui , kwani nafikiri inayojulikana ni Taifa star..au nimekosea?