Member of EVRS

Tuesday 16 November 2010

Pinda athibitishwa kuwa Waziri Mkuu Tanzania


Mhesh Kayanza Mizengo Peter Pinda leo jioni amethibitishwa na Bunge kuwa waziri mkuu wa Tanzania baada ya kupata kura za ndiyo 277 sawa na asilimia 84.5 ya kura halali zilizopigwa, na pia kura 49 za hapana sawa na asilimia 14.9
  
Mhesh Pinda anatarajiwa kuapishwa kesho ikulu ndogo ya Chamwino iliyopo Dodoma. Na hapo baadaye yeye kwa kushirikiana na Rais Kikwete na pia makamu wa Rais, Dk Bilal wataandaa baraza jipya la mawaziri.  
  
Watu wengi walikuwa wanatarajia uteuzi wa Pinda kuwa waziri mkuu wa Tanzania.  
   
Hatuna budi kumpongeza, tukitumaini ya kuwa atatenda majukumu yake kama kiongozi wa serikali bungeni vyema na kupigania haki ya watanzania wote na sio maslahi ya chama chake.  
 
Mungu ibariki Tanzania.

2 comments:

Simon Kitururu said...

Fanya kweli basi Mkuu Pinda watu tukuenzi kikwelikweli.


Si unajua hongera za kabla ya kazi KUFANYIKA ni kuvimbishana vichwa tu kwa hewa?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

jamaa mwana si-hasa kweli huyu, anajua kuongea ila matendo!