Member of EVRS

Sunday 7 November 2010

Kenya: Polisi aua watu 10 Kwa Kinachodhaniwa ni Wivu wa Mapenzi

Jumamosi usiku, Mji wa Siakago ambao upo kama km 150 kutoka Nairobi uligeuka kwa muda kuwa uwanja wa kumwaga risasi mara baada ya afisa wa polisi mmoja kwenda kwenye baa moja ikisemekana alikuwa na nia ya kumfuata rafiki yake wa kike ambaye alidhani atakuwa kwenye baa hiyo.  
   
Baada ya kumkosa alifyatua risasi humo na kuua mtu mmoja, baadaye akaenda baa ya pili na kufyatua tena risasi ambapo aliua tena mtu mmoja. Na mwisho alienda baa ya tatu, alipomkosa akafyatua tena risasi na kuua watu wanane hapo.   
    
Habari ambazo hazijathibitishwa rasmi, zinasema kati ya waliouawa, wawili ni polisi.
Chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana, ila inasemekana muuaji huyo alijisalimisha mwenyewe kituo cha polisi, na alidai alifanya hivyo baada ya kuishiwa risasi.  
  
Polisi walikuwa wamemuweka chini ya ulinzi mkali katika kituo kikuu cha polisi, Embu. 
   
Ndugu na jamaa waliopoteza ndugu zao walikuwa katika taharuki na gadhabu kubwa kwa tukio hilo, kiasi kwamba usalama wa mtuhumiwa na kituo alichohifadhiwa kilikuwa hatarini kushambuliwa.  
   
Polisi bado wanaendelea na uchunguzi, huku habari za rafiki wa kike wa muuaji hazijulikani, kwani katorokea mahali pasipojulikana.  
  
Watu wengi hawakuwa na habari kuhusiana na kilichokuwa kinaendelea, huku wakidhani ni sherehe za wahindu kusheherekea sikukuu ya Diwali zikiendelea, ambazo huambatana na urushaji wa fataki na milipuko.

3 comments:

emu-three said...

Haya mambo bwana yasikie tu, hayana cha mlinda usalama, raisi au mkuu wa dini...wivu ni hatari!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ila ssasa, ataua amlindaye kama raisi ua PM

Simon Kitururu said...

:-(