Jana nilizungumzia kizunguzungu cha siasa za Kenya.
Nafikiri sikukosea sana, pale niliposema ukitaka kuchanganyikiwa, basi fuatilia kwa moyo wako wote siasa za Kenya.
Kitendo cha kumualika kisiri siri rais wa Sudan, Al Bashir, ambaye anatafutwa na mahakama ya waalifu ya the Hague kwa kutuhumiwa kuamuru mauaji ya kimbari huko Darfur, kiliziudhi duru za nchi kadhaa za Ulaya na Marekani.
Habari mpya iliyopatikana, inadai kwenye orodha ya wageni mashuhuri waliokuwa wamealikwa, Al Bashir hakuwemo, ila rais wa Sudan Kusini ndiye aliyekuwa ameorodheshwa.
Na pia wakati Al Bashir anaingia viwanja vya uhuru park, hakutambulishwa kama walivyofanya kwa viongozi wengine. Cha kushangaza zaidi wageni wengi waliduwaa kumuona Al Bashir hapo.
Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Koffi Annaan, naye pia alionekana kushangazwa na uwepo wa Rais huyo wa Sudan.
Pia inasemekana kuna baadhi ya mabalozi waliokuwepo hapo viwanjani, ilibidi wavutane kando kujadili jambo fulani baada ya Al Bashir kuwasili.
Labda kipya zaidi, ni pale Waziri mkuu wa Kenya, Raila, naye aliposema ya kuwa hakuwa na taarifa ya kuwa Al Bashir alialikwa, alishtukia tu kumuona katika tukio hilo?!!!
Msemaji wa serikali ya Kenya, anatetea kumualika Al Bashir, ya kuwa inadumisha amani katika eneo lao na majirani zao.
Baadhi ya wakenya walisema waliudhiwa na kitendo cha kuwepo kwa Al Bashir kwenye sherehe za kuzindua katiba mpya, kwani alimaliza furaha yao waliyokuwa nayo
Tanzania iliwakilishwa na rais wa Zanzibar, Karume.
Uzushi: Inakuwaje wageni maarufu kualikwa wakati waziri mkuu hana habari kabisa.... Na kwa nini Kenya haikumtangaza Al Bashir wakati anaingia?.
Na je? Kwa nini Kenya ilidanganya ya kuwa walikuwa wamemualika rais wa Sudan Kusini wakati mambo hayakuwa hivyo?
Ndio siasa za Kenya hizo, bil migogoro... haziendi
3 comments:
Lakini kama ni sawa kukamatwa nafikiri tungeanzia kwa Bush mwenyewe, aliua watu Iraq, na silaha hazikupatikana, yeye na Albashir lao moja
eti ehe, siasa ni ujinga fulani, tuanze na Bush, blair nk, then sudan baadaye
ukiona wadhungu wanamwandama mtu, hujue kawachomolea maslahi au hataki ukoloni nchini kwake
ha ha haaaa
Post a Comment