Member of EVRS

Tuesday, 31 August 2010

OSEA Conference 2010, Dar es Salaam - Tanzania

Ophthalmological Society of Eastern Africa (OSEA) had its 39th Annual Conference held at Golden Tulip Hotel in Dar es Salaam, Tanzania.
It was one of the successful meetings despite being overwhelmed by conference visitors more than the expected number. Tanzanian team worked relentlesly through out .....

Eastern Africa region includes Burundi, Ethiopia, DRC, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda, and Zambia. Malawi has been invited, but they havent officially joined the OSEAPhoto above: Registration in process
Madhumuni makubwa ya mkutano huu ilikuwa ni kufanya marejeo ya mpango wa kutokomeza upofu kwa miaka 20 ufikapo mwaka 2020, na kuangalia kama tunakwenda sambamba na malengo yaliyokusudiwa baada ya kumaliza nusu ya kwanza ya mpango huo.
Hakuna kusubiri muda uishe ndio kuanza kuangalia kama tumefanikiwa au la!
Mbali ya watu kuandaa na kuanuisha tafiti mbalimbali na mafanikio ya kazi zao katika nchi zao.
Mwishoni, walichaguliwa viongozi wapya wa shirikisho hili la ukanda wa Afrika mashariki kama ifuatavyo:
Dr. Dan Kiage (Kenya) - Chair person
Dr. Amir Bedri (Ethiopia) - Vice Chair
Dr. Edward Nkurunziza (Uganda) - Secretary
Dr. Chibuga (Rwanda) - Vice Secretary
Dr. Ibrahim Matende (Kenya) - Treasurer


Dr. Kilima and Dr. Hassan, who are the vice chair and Chair of OSEA -Tanzania respectively discussing the event proceedings

Dr Bernadetta Shilio-Mpoki who is deputy National eye care co-ordinator and onchocerciasis programme at the Tanzania's Ministry of Health and Social Welfare ( And my former classmate at undergraduate) listening careful the proceedings of the conference

Wajumbe mashuhuri kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania wakisikiliza mkutano kwa makini

Nami sikuachwa nyuma, nilikuwepo

Multi-Nation presenters at the time of Questions and Answers after session 6

Invited guest speakers from Germany, during questions and answers session 7

Baada ya mkutano kwisha, kulikuwa na tafrija ya kufahamiana zaidi huku kukiwa na kiburudisho cha muziki "live". Hapo ndipo watu wengine waliendelea kuonyesha vipaji vyao....lol :-)

Monday, 30 August 2010

Yaliyojiri Baada ya Al Bashir kuwepo Kenya

Jana nilizungumzia kizunguzungu cha siasa za Kenya.

Nafikiri sikukosea sana, pale niliposema ukitaka kuchanganyikiwa, basi fuatilia kwa moyo wako wote siasa za Kenya.

Kitendo cha kumualika kisiri siri rais wa Sudan, Al Bashir, ambaye anatafutwa na mahakama ya waalifu ya the Hague kwa kutuhumiwa kuamuru mauaji ya kimbari huko Darfur, kiliziudhi duru za nchi kadhaa za Ulaya na Marekani.

Habari mpya iliyopatikana, inadai kwenye orodha ya wageni mashuhuri waliokuwa wamealikwa, Al Bashir hakuwemo, ila rais wa Sudan Kusini ndiye aliyekuwa ameorodheshwa.

Na pia wakati Al Bashir anaingia viwanja vya uhuru park, hakutambulishwa kama walivyofanya kwa viongozi wengine. Cha kushangaza zaidi wageni wengi waliduwaa kumuona Al Bashir hapo.
Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Koffi Annaan, naye pia alionekana kushangazwa na uwepo wa Rais huyo wa Sudan.
Pia inasemekana kuna baadhi ya mabalozi waliokuwepo hapo viwanjani, ilibidi wavutane kando kujadili jambo fulani baada ya Al Bashir kuwasili.

Labda kipya zaidi, ni pale Waziri mkuu wa Kenya, Raila, naye aliposema ya kuwa hakuwa na taarifa ya kuwa Al Bashir alialikwa, alishtukia tu kumuona katika tukio hilo?!!!

Msemaji wa serikali ya Kenya, anatetea kumualika Al Bashir, ya kuwa inadumisha amani katika eneo lao na majirani zao.

Baadhi ya wakenya walisema waliudhiwa na kitendo cha kuwepo kwa Al Bashir kwenye sherehe za kuzindua katiba mpya, kwani alimaliza furaha yao waliyokuwa nayo

Tanzania iliwakilishwa na rais wa Zanzibar, Karume.

Uzushi: Inakuwaje wageni maarufu kualikwa wakati waziri mkuu hana habari kabisa.... Na kwa nini Kenya haikumtangaza Al Bashir wakati anaingia?.
Na je? Kwa nini Kenya ilidanganya ya kuwa walikuwa wamemualika rais wa Sudan Kusini wakati mambo hayakuwa hivyo?

Ndio siasa za Kenya hizo, bil migogoro... haziendi

Sunday, 29 August 2010

Insanity of Politics: Kenya's perspective

If you want to become mad, then assumes yourself as a greatest Fan of Kenya's politics!..... Probably politics in general.

Some leaders, they are just like flags, they are highly driven by political wave, whether it resemble hurricane, see breeze or just normal wind... They cannot control themselves.

Within few years, politicians in Kenya had several ties and breaks. All ties and break-ups are just influenced by the country's political waves.

I dont want to recall post-election violence which claimed several souls of many innocent people. Kibaki ang Raila had a great tabloid situation based on politicl cheats on vote counting. Through externa forces, the two politicians eventually settled their "bills".

Two allies then clashed again on issues related to ministers who were thought to be mafisadi. Raila suspended them, but Mwai surfaced on another side of the coin and nullified Raila decision.

When the issue of Katiba became hot, the two top comrades became friends again, and one minister who was pardoned by Kibaki, went against Kibaki on this constitution issue!!

Well, well, eventually many people supported the new constitution which was ratified on 27th August 2010.

Mwai Kibaki after signing the new constitution ( Photo by world bulletin)

The day for ratification of Kenya's new constitution, Omar Al-Bashir of Sudan was invited which angered United Nations. US president also was not satisfied with this act.

I still wonder the man below (Photo by Reuters) whose thinking assumes Obama plus Oginga and Kibaki makes a new Kenya... while Obama was angered by Kenya's to invite Al Bashir....

The day of inauguration of new constitution, people they gathered at Uhuru Park from 5.00 am ( I just wish all workers will be punctual at their respective offices like this)

Interestingly, some VIP/ministers, they failed to get chairs. Master of ceremony had to work hard to secure more chairs for the VIP.

At the ground, noises and vuvuzelas were the Kachumbari of the day!

We are waiting to hear something nutty from there!!!

Wednesday, 25 August 2010

Sababu za Vita Kwenye Kuwania Ubunge Tanzania


Kwa wale ambao hawakupata bahati ya kusoma gazeti hili .....
Ukisikia vita ya kisiasa Tanzania, basi ujue sababu ndizo hizi.......
Ukumbuke pia, wanasema posho hazitoshi, na wanataka nyongeza. Achilia mbali kuitwa muheshimiwa, kamati za Bunge nk.
Ni wachache tu ndio wana dhamira ya kweli ya uwakilishi wa wananchi. Wengine wanawakilisha wenye nchi!!

Tuesday, 24 August 2010

Pakistan: Situation Worsening

Aerial Photo: NASA

Pakistan is facing the most difficult time ever seen before.

It seems flooding is unlikely to stop soon.

Everything moves upside down. Displacement of people is no more an issue to think, but rather thinking who and how will people survives.

When you survive from floods, you pave your way into starvation and diseases, cholera is building up.

Hospitals have no more electrical power, there is no sufficient medical supplies, no clean and safe water, no food, insufficient aid workers.

Emergency surgical operations at night have to be done under candle lightening.

Deliveries are carried by using repeated cleansed gloves..... barerly with water. You can still see traces of blood on cleansed re-usable gloves.

What a mess!!!!

Pakistani .... they need every possible help to survive.

Tuesday, 17 August 2010

Safari


I will be away for a while.
I am travelling to attend important conference.

Nina matumaini tutakuwa pamoja pindi muda utakaporuhusu.
Tuendeleze mshikamano

Sunday, 15 August 2010

Orodha ya Wagombea Ubunge wa CCM - 2010

Orodha ya wana CCM walioteuliwa kugombea ubunge mwaka 2010 bofya hapa kwa Subi uipate yote.

Kilichonishangaza ni mchanganuo wa elimu zao, wengine wameandkiwa elimu ya msingi, wengine darasa la saba. Wengine sekondari, wengine kidato cha tatu, nne, sita nk. Sikuelewa mantiki hii.

Tofauti ya darasa la saba na elimu ya msingi?!!!

Kazi kwako

Blank Sunday


Today, every thing seems to be so quiet.
After continuous .... very busy 14 days, it seems I am still exhausted, I feel as if I am not in a mood to relax outdoors, rather I prefer to lie down and close my eyes.
The lovely scenes I always like to see, appears as if they are on the other side of my sight.
Everything looks empty, motionless and soundless.
That is the best way of explaining how tired somebody can be.
The best thing.. is that, we are safe and sound.
My Holiday is approaching, I cant wait...
Thanks for reading my short note .... I Wish you a lovely Sunday!

Thursday, 12 August 2010

Rwanda Vipi tena?!! Grenade attack!

You can get info in English here

Wakati watu wakianza kusheherekea ushindi wa Kagame, mara baada ya tume ya taifa ya uchaguzi kutangaza ushindi wa Kagame wa asilimia 93 hapo jana. Kufika saa moja jioni .. mara BOOOOOOM

Yaani watu wakarusha gruneti katika mtaa na nyakati ambapo watu huwa wanakuwa wengi wakitokea kazini kuelekea nyumbani, tena kwenye kituo cha mabasi ya usafiri wa jiji la Kigali, nikilinganisha na mabasi ya daladala labda katika kituo cha Kariakoo muda wa jioni.

Mlipuko ulikuwa mdogo, lakini ulijeruhi watu zaidi ya 7 na wengine kadhaa kupata majeraha madogo madogo.

Watu wengi hawakuwa na habari ya tukio hili, mimi nikiwa mmoja wapo, kwani nakaa mbali kiasi na mjini, na pia nimefunga matembezi ya jioni sana na usiku hasa sehemu za misongamano.

Kwa leo mji umetulia kabisa, huwezi kujua hata kama kulikuwa na tukio lolote. Maisha yanaendelea kama kawaida.

Tuesday, 10 August 2010

Rwanda: Wakesha Kwa Bashasha na Sherehe

Wanyarwanda jana usiku wamekesha kwenye uwanja wa Taifa - Amahoro wakipokea matokeo kutoka sehemu mbalimbali ya kura za rais.


Naweza kusema kuwa karibu wote waliokuwepo kiwanjani walikuwa wapenzi wa RPF ambacho ndio chama cha Rais wa sasa Paul Kagame. Uwanja ulikuwa umejaa na kutapika kwa idadi ya watu.


Shughuli hiyo ya kupokea matokeo moja moja, ilikuwa inaonyeshwa na Televisheni ya Rwanda, na uwanjani watu walikuwa wanashuhudia kwenye screen kubwa na kushangilia vilivyo.


Sherehe hizo maarufu kama "Hakuna Kulala" ziliendelea kuanzia saa 12 jioni hadi asubuhi. Rais Kagame naye pia alihudhuria sherehe hizo.

Matokeo rasmi bado hayajatangazwa na tume ya uchaguzi, kwani bado inaendelea kupokea matokeo. Mwelekeo unaonekana Kagame atashinda kwa zaidi ya asilimia 95.


Leo nikiwa tayari kwenda kazini, kabla sijatoka, nimetaarifiwa kuwa leo ni siku ya mapumziko. Sijajua ni mapumziko ya kusheherekea ushindi, au watu wamechoka kwa kukesha usiku mzima wakishangilia au........ duh!


Imenibidi nitundike madaluga, nikikusanya nguvu, kwani kesho nitakuwa na kibarua mara 3 zaidi ya siku zote, kwani kazi za siku 2 zimelala, ukiongeza na kesho.. lah, laiti ningejua mapema ...........

Monday, 9 August 2010

Rwanda: Uchaguzi Wa Rais Waenda kwa Amani

Wananchi wa Rwanda Leo wamekuwa wanapiga kura za kumchagua rais wao kwa kipindi cha miaka saba (7) kutoka sasa.

Kiongozi wa sasa, Paul Kagame, anatarajiwa kupata ushindi wa mteremko kutokana na joto la kampeni lilivyokuwa likienda kwa takribani wiki 6 tu. Pia bado anakubalika na wananchi wengi.
Kagame alichaguliwa kwa mara ya kwanza kwenye uchaguzi wa vyama vingi miaka saba iliyopita, na alipata ushindi mkubwa sana.


Picha ya juu. Watu walipokuwa wakiingia na kutoka katika kituo cha kupigia kura leo asubuhi karibu na ninapokaa.
Upigaji wa kura unatazamiwa kusitishwa saa tisa alasiri, na shughuli za kuhesabu kura zitaanza mara moja.
Vituo nilivyotembelea kwenye muda waa saa 6 adhuhuri, nilikuta vimebakia na wapiga kura wachache, kwani inakadiriwa kwa kila kila chumba kimoja cha kupigia kura, kinatarajiwa kuwa na wapiga kura 50.
Pia kila kituo, kilikuwa kinapiga nyimbo za kuhimiza watu watumie haki yao ya kidemokrasia kupiga kura. Askari vituoni hali kadhalika walikuwa sio wengi, ukilinganisha na usiku wa kuamkia leo ambapo kulitanda askari wa jeshi la ulinzi na polisi wakipiga doria kila kona.
Jana usiku ndio ilitangazwa ya kuwa leo itakuwa ni mapumziko ili watu wapige kura, vinginevyo nasikia utaratibu wa zamani ilikuwa ni kupiga kura na kuelekea kazini.
Tunatarajia matokeo kutangazwa si zaidi ya tarehe 17 mwezi huu kadiri ya ratiba ya tume ya uchaguzi.
Uchaguzi wa wabunge ulisha fanyika, kwani wabunge huchaguliwa kila baada ya miaka 5 na Rais ni miaka 7.

Friday, 6 August 2010

Weekend, weekend!


Despite that this bird was making mess on my trees, but will not make me fail to say .... have a lovely weekend.
Keep in touch before another monday!

Tuesday, 3 August 2010

Sunday, 1 August 2010

Lovely Sunday


Nimetingwa na kazi mpaka nimeshindwa kuandaa chochote cha kubadilishana mawazo nawe!
Jaribu kunikumbusha, au kubahatisha hapa ni wapi, maana nilishaondoka hapo kitambo
Nakutakia Jumapili njema!