Member of EVRS

Thursday 8 October 2009

Kenya: Bomu Linalosubiri Muda Muafaka

Kumekuwa na fununu kuwa baadhi ya wananchi Kenya wameanza kukusanya silaha za moto kama maandalizi ya kujihami na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 1012.
Na pia kumekuwa na ongezeko kubwa la uhalifu kwa sasa, na matukio yamekuwa yakiongezeka kila siku.

Uchunguzi uliofanywa na BBC umebaini ni kweli kuwa watu wameanza kununua silaha, na hasa kutoka Somalia, na hata baadhi yao walipo hojiwa walikiri kuwa wameshanunua kwa nia ya kujihami.

Serikali ya Kenya imekuwa inapinga ya kuwa matukio kama hayo hayapo, isipokuwa imekubali ya kuwa matukio ya uhalifu yameongezeka.

Swali kubwa ninalojiuliza, je, ni kweli serikali ya Kenya ipo makini na suala hilo, au watendaji wanafurahia hali ya vurugu wakati wa uchaguzi ili waweze kufanya "mambo yao"!

Ikumbukwe, wanaoumia siku zote ni watu wa kawaida na wasio na hatia, wakati viongozi na wachochezi wa vurugu huwa salama salimini. Hatupendi hizo kafara za uchaguzi EA.

1 comment:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ni kweli. Kuna familia kadhaa nazijua wameshanunua nyumba Tanzania na wanategemea kuhamia Tanzania kwa muda mpaka uchaguzi utakapopita. Kuna wasiwasi mkubwa sana. Natumaini kwamba Watanzania hatutafikia hatua hii.