Member of EVRS

Thursday, 1 October 2009

Education or Add question?!!!

This pupils... The only thing they enjoy in this classroom is the outside view.....
And sitting very close to the writing board is unhealthy!!

Baada ya hapo tunategemea watoto wetu waweze kufanya vizuri kama wale ambao wana kila kitu cha kuwasaidia kupata elimu. Kinachonitisha zaidi ni jinsi walivyokaa karibu kabisa na ubao, maana yake wakitumia chaki kuandika halafu mtu afute... vumbi lote linaingia ndani ya macho na pua, baada ya hapo wanapotea darasani wakiwa wagonjwa.

12 comments:

Simon Kitururu said...

Kazi tunayo!:-(

Yasinta Ngonyani said...

Pamoja na kukosa sehemu nzuri ya kukaa lakini watoto wanaenda tu shule. Ila sidhani kama hapo kinaingia kitu kichwani. Inasikitisha sana na sijui serikali inafanya nini? Ufisadi tu, kuchukua pesa na kuwapeleka watoto wao kwenye shule nzuri.Naacha isije nikasema nisichotaka kusema.

Anonymous said...

Hii ni balaa ya baradhuli. Poor pupils!!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Pamoja na kusoma katika mazingira magumu namna hii, pamoja na kufundishwa katika lugha ambayo siyo yao na pengine wasiyoifahamu vizuri, pamoja na kuwa na kazi nyingi nyumbani kiasi kwamba hawana muda wa kujisomea, pamoja na kufundishwa na walimu ambao wenyewe pengine hawana uhakika sana na wakifundishacho kwa sababu nao hawakufanya vizuri katika mitihani yao (ndiyo maana wakaishia kuwa walimu), pamoja na ukweli kwamba pengine baadhi yao hapo walipo wana njaa, pamoja na kwamba pengine wengine ni mayatima na hawana familia zenye upendo, pamoja na...watoto hawa bado wanakwenda shuleni kwa sababu wanaamini kwamba elimu pekee ndiyo itakayowakomboa. Na kweli utakuta baadhi ya watoto hawa wanasoma mpaka kufika chuo kikuu. Je, ingekuwaje kama wangekuwa na kila kitu kama wenzao katika sehemu nyingine duniani?

Na pengine swali la msingi ni hili: ni kweli nchi yao ni masikini kiasi kwamba haiwezi kuwanunulia angalau vidawati vya kukalia? Au wajanja wachache weshatumia pesa za kununulia vidawati kujijengea mahekalu au kwenda vekesheni Ulaya na familia zao? Kuna anayewaonea uchungu? Nani awapiganie?

Mzee wa Changamoto said...

Nanukuu swali la Profesa kuwa "ni kweli nchi yao ni masikini kiasi kwamba haiwezi kuwanunulia angalau vidawati vya kukalia?"
Jibu ni kuwa WATAWALA WAO NDIO MASKINI WA FIKRA NA AKILI ZAO WASIOJUA KUWA WANACHOPUUZA KUWEKEZA NDICHO CHA MUHIMU KULIKO MARADHI WANAYOJITAFUTIA KWA KUJILIMBIKIZIA MALI NA KULA VISIVYOHITAJIKA MIILINI MWAO.
Kiama chao chaja.

ARO GERALDES said...

Beautiful picture! It's exciting to see the kids studying, defying the odds to build a better future.
My best regards from Buenos Aires
Pablo Aro Geraldes, an Argentine friend...

chib said...

Nakubaliana na wote, nchi zetu zimekuwa maskini kwa umaskini wa fikra za hao wanaoitwa viongozi.

Pablo, you are welcome!

Anonymous said...

調子が悪いです。 [url=http://ci2s.org/viagura.htm]バイアグラ[/url] バイアグラ 個人輸入

Anonymous said...

Ich tue Abbitte, es kommt mir ganz nicht heran. levitra viagra generika [url=http//t7-isis.org]viagra ohne rezept[/url]

Anonymous said...

me parece esto la frase magnГ­fica http://nuevascarreras.com/cialis/ comprar cialis en mexico Come curiosi .. :) [url=http://nuevascarreras.com/tag/cialis-online/ ]comprar cialis generico [/url]

Anonymous said...

Claro sois derechos. En esto algo es y es el pensamiento excelente. Es listo a apoyarle. http://nuevascarreras.com/tag/cialis/ cialis E vi ГЁ un altro modo? [url=http://nuevascarreras.com/ ]cialis generico comprar [/url]

Anonymous said...

Pienso que no sois derecho. Soy seguro. Lo discutiremos. [url=http://csalamanca.com/tag/comprar-viagra/ ]viagra 100 mg pfizer [/url] Todo sobre uno y tan infinitamente http://csalamanca.com/tag/comprar-viagra/ viagra generico comprar