Member of EVRS

Wednesday 4 July 2012

Rwanda Yaadhimisha Miaka 18 Baada ya Mauaji ya Kimbari ya Mwaka 1994


Siku ya leo tarehe 4 Julai 2012, Rwanda imeadhimisha miaka 18 tangu mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi yalipomalizika. 
Tarehe kama hii ya leo hapo mwaka 1994, jiji la Kigali lilikombolewa na majeshi ya RPF na hivyo kukomesha mara moja mauaji yaliyokuwa yanaendelea amabyo yalilengwa haswa kwa watutsi, japo na wale wahutu wenye msimamo wa wastani nao walikuwa wakishambuliwa na hata kuuawa. 
  
Siku kama ya leo, watu huwa wanatoa ushuhuda wa matukio yalivyokuwa na kuendelea kutoa msamaha kwa wale waliofanya mauaji na kutesa watu waliokuwa hawana hatia. 
  
Tarehe 4 Julai huwa ni kilele cha maombolezo ambayo huanza tarehe ambayo ni sambamba na wakati mauaji yalipoanza mnamo mwezi wa Februari. 

Kwa mwaka huu wa 2012, wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka nchi za Kenya, Tanzania, Uganda na Burundi waliungana kwa pamoja kwenda kutoa heshima kwa wahanga wa mauaji hayo waliozikwa kwenye eneo la Gisozi wakisindikizwa na wanyarwanda ambao wengi wao walikuwa wakiishi Tanzania kama wakimbizi baada ya kukimbia vita na mauaji ya kikatili yaliyokuwa yakiendelea wakati huo nchini Rwanda. 

2 comments:

emuthree said...

Hii kiswahili safi tuatsema wanaadhimisha, mimi naona kwenye kiswahili jambo lakukumbuka la huzuni tuliite `wanaomboleza, au wanakumbukia...'kuadhimisha inakuwa kama jambolafuraha, kama vile kupata uhuru...ni wazo tu!

Yasinta Ngonyani said...

Twawatakieni amani na upendo tele!!