Member of EVRS

Thursday, 2 February 2012

Breaking News: Ajali Mbaya ndani ya Shule ya Sekondari ya wasichana ya Korogwe

Gari dogo aina ya Toyota limewagonga wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe wakati wakiwa katika mahafali ya wanafunzi wenzao wa kidato cha sita. Ajali hiyo imetokea chini ya nusu saa kutoka ninapoandika habari hii.  
  
Zaidi ya wanafunzi 10 wamejeruhiwa vibaya, na wanne kati ya hao wameumizwa na hawana fahamu wala kuonyesha dalili yoyote ya uhai. Bado hawajathibitishwa kama wako hai au wamekwisha fariki. 
  
Hilo gari lililowagonga, linasemekana lilikuwa limewaleta baadhi ya wazazi wa wanafunzi. Pia inasemekana lilikuwa katika mwendo kasi mkubwa wakati lilipoingia ndani ya eneo la shule.
Habari zaidi zitawasilishwa baadaye

2 comments:

Subi Nukta said...

Kaka, asante kwa taarifa. Naomba tufahamishe majina na ikipidi picha tafadhali. (muhimu kweli kwangu).

emu-three said...

Inasikitisha kweli, hiyo ndio ajali..