Suala la upatikanaji wa umeme, Watanzania inabidi waendelee kuishi kwa matumaini…
Kampuni inayozalisha gesi asilia kutoka visiwa vya Songosongo, Songas imekiri kuwa haina uwezo wa kuzalisha gesi ya kuendesha mtambo mpya ulionunuliwa na Tanesco wa kuzalisha umeme wa megawati 100 kwa kutumia gesi asilia.
Kampuni hiyo imesema kwa sasa inazalisha gesi kwa kiwango cha ukomo wa juu, na haiwezi kuongeza hadi itakapofanya upanuzi wa mitambo yake ya kuzalisha gesi ikiwa ni pamoja na kubadili bomba la kusafirisha gesi kuelekea Dar es Salaam. Shughuli hii inatarajiwa kukamilika baada ya miaka 2. Kwa maana hiyo, hata hizo megawati za ziada kutoka Tanesco zitapatikana kuanzia mwaka 2013. Hii ina maana huo mtambo ambao Tanesco ilikimbilia kuununua haraka haraka utakaa bila kazi hadi mwaka 2013!!!!!
Hii inanikumbusha hotuba za mbunge wa CHADEMA na waziri kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika. Pia na ile ya mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini, January Makamba (CCM), ambao walionyesha shaka kubwa kwa mipango ya Tanesco katika kuzalisha umeme huku wakiwa hawajajipanga kujua ni wapi watapata nyenzo za kuendesha hatua zao za dharura.
Sasa ukweli umeanza kujionyesha kuwa mipango ya hawa wenzetu ni kweli ilikuwa ni ya “zima moto” kwa maana zote mbili za kufanya mambo kidharura ambapo mara nyingi watu hawafikirii sana zaidi ya kuuzima moto haraka kabla haujaharibu zaidi, na pili kufanya mchezo wa kiini macho kuwapumbaza watu kuwa umeme waja hivi karibuni kupunguza moto wa hasira za watu na wabunge kuhusiano na mgao mkubwa giza…
Lakini…. Walikuta wabunge karibu wote bila kujali itikadi zao za kisiasa, walikuwa tayari ni moto usioweza kupozwa kwa mbinu ya ghiliba.
Watanzania endeleeni kuishi kwa matumaini mkitegemea mgao wa mbalamwezi, kwani hata hizo taa za mafuta ya taa mtashindwa kuzitumia baada ya bei ya mafuta ya taa nayo kupandishwa. Siku mkipata umeme kwa siku nzima inabidi mshangae
5 comments:
Kwasababu rais wetu ametuthibitishia kuwa serikali yake haina uweza kufanya mvua inyeshe!
Duuuh, najiuliza kama wazee wtu wasingeweza hata kuianzisha hiyo Tanesco tungekuwaje, maana hata hicho kilichoanzishwa tunashindwa kukiendeleza...kweli tupo `hopulesi'
Kweli Kabisa emu-three
Safari ndefu tunayo
mhhhhh
Post a Comment