Member of EVRS

Tuesday, 2 August 2011

Indonesia: Matibabu kwa Njia ya Mshtuo wa Umeme (Treatment using Electric shock)

Watu wa Indonesia wamekuwa wanatumia njia ya kujilaza kwenye njia za reli ili wapate mshtuo wa umeme kwa nia ya kupata matibabu ya maradhi mbalimbali hasa yanayohusiana na uchovu (Relaxing spa treatment). 
  
Wanachotarajia ni kupata mshtuo mdogo wa nguvu za umeme kutoka kwenye reli hizo hasa njia hiyo inapotumika na zile treni za umeme zilizounganishwa kwa waya za juu. 
Inasemekana wakati mwingine unahitaji kukaa kwa muda wa karibu saa moja kwenye reli za uvuguvugu, maana yake ni lazima ulale juani ili kuweza kupata mshtuo huo. Waliojaribu, wanasema kuna wakati inaogofya kwani mshtuo wa umeme (electric shock) unaweza kuwa na nguvu kidoogo kiasi cha kuleta msisimko ule mtu anaoupata akishika transistor.  
  
Matibabu haya yamekuwa yakikatizwa mara nyingine na treni zinazokuja kwenye njia hizo na kuwalazimu watu kutimua mbio (kukimbia) ili wasije wakagongwa.  
   
Shirika la reli la Indonesia limejitahidi kuzuia watu bila mafanikio na kufikia hatua ya kuweka vibao vya tahadhari likiwaonya watu wanaojilaza kwenye reli ya kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai.  
  
Hii ni changamoto kwa Tz..... umeme kwa matumizi ya kawaida tu ni kwa mbinde, sasa......

Picha kutoka Aol Travel

2 comments:

emu-three said...

Du mkuu hiyo mpya...sisi huku tunavyoogopa umeme, ....labda kwa vile umeme wetu ni wa MGAWO, hatujauzoea sana, unakuja kwa vipindi KAMA HOMA YA KUPANDA NA KUSHUKA. TUPO PAMOJA MKUU

Goodman Manyanya Phiri said...

Umoja Wa Mataifa ingilie kati jambo hilo. Inamaana nchi hiyo inashida kiasi kwamaba wagonjwa wako tayari vile kufa na umeme kwa ukosefu wa tiba? UJINGA!!!