Member of EVRS

Friday, 26 August 2011

Donald Trump and His New 100$ Millions' Private Jet

 Bilionea Donald Trump hivi karibuni alinunua ndege yake binafsi kutoka kwa Paul Allen kwa jumla ya dola za kimarekani kama milioni 100. Ndege hiyo aina ya Boeing 757 ni ya kisasa zaidi.
 Ina uwezo wa kuchukua kama watu 53. Na imepambwa kwa vitu vilivyopakawa rangi ya dhahabu ikiwa ni pamoja na mikanda ya usalama.
 Ina sehemu ya maongezi ya faragha au mkutano, kuna sehemu ya kupumzika, pia ina mfumo wa kisasa wa muziki na televisheni.
 Mbali ya hayo, ina sehemu ya jiko iliyotengenezwa kwa nakshi za mbao na masinki ya marumaru ya kahawia na mabomba yaliyopakawa utando wa dhahabu. Bafu na choo pia vimo....
Ndani ya ndege hii, kuna kitanda kikubwa cha kulala, ambapo Bw Donald akiwa anasafiri, anaweza kupumzika kwa amani.

Wanasema maisha ni mafupi, kama unazo, basi ni lazima ujipe furaha ukiwa katika Dunia hii, ambapo ni mapito tu ya watu!

For more information, click here, na ukitaka kuona video yake, basi bonyeza hapa

4 comments:

Fadhy Mtanga said...

duuuh! kweli duniani kuna watu ambao wanaishi na wanajua kuishi.

SIMON KITURURU said...

Lakinin nimesikia mahali ukifurahi sana hapa DUNIANI labda hiyo ni dalili hufanyi yaelekezayo watu MBINGUNI kwa kuwa ajuaye matamu ya BINADAMU kidunia nasikia ni SHETANI na ndio maana mengi wapendayo WANADAMU nidhambi!:-(

emu-three said...

Mmmh, kweli tajiri kuingia mbinguni ni nini vile....maana unanunua ndege watu Somalia na wapi kule wanakufa kwa njaa...kweli dunia ni mviringo!

Amin said...

This is very interesting...