Member of EVRS

Monday 15 August 2011

Wananchi wa Kigamboni Waelekea Kuufukuzia Mbali Mradi wa Mji Mpya


Katika hali inayoonyesha kupungua kwa imani na kukata tama kuhusu ahadi ya ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni, pia kuchoshwa na ahadi za serikali iliyopo madarakani, wananchi wa Kigamboni wamemuagiza mbunge wao Mhesh Dr. Faustine Ndugulile aufikishe ujumbe wao kwa waziri wa Ardhi, ustawi wa maliasili na maendeleo ya makazi ya kuwa wamechoshwa na subira ambayo hatima yake haijulikani. 

   
Hii ni kutokana na kuwa serikali ilisitisha shughuli zote za kuendeleza makazi na matumizi ya ardhi katika baadhi ya maeneo ya Kigamboni ili kupisha ujenzi wa mji mpya ambao unatarajiwa kujengwa eneo hilo la Kigamboni. Amri hii ya katazo ilitolewa tangu mwaka 2008 na ilikuwa imepangwa kuwa mpango wa ujenzi uwe umeanzwa ndani ya muda wa miaka 2 tangu ilipotolewa amri ya kusitisha shughuli zote za maendeleo. 
  
Kutokana na serikali kushindwa kuainisha ni lini kazi hiyo ya ujenzi wa mji mpya itaanza ikitanguliwa na kufanya uthamini wa mali za watakaoathirika, sehemu mbadala watakapokwenda kuishi ili kupisha ujenzi huo na muda wa kulipwa fidia. 
  
Kwa sababu serikali imekaa kimya kwa muda mrefu, huku wakazi wa eneo hili wakishindwa kuendeleza makazi, au kuuza maeneo yao wahamie kwingine, wameamua kumuagiza mbunge wao ampatie taarifa waziri Tibaijuka ya kuwa ifikapo tarehe 30 June 2012, kama Serikali haitakuja na mpango madhubuti wa kueleza kwa uhakika muda wa shughuli zote za upanuzi wa mji ukiwa na fidia, basi huo mradi wasiulete tena Kigamboni, na watafute sehemu nyingine kwa watu wasiojua maendeleo ni nini ndio wawapelekee. 
  
Mbunge wa Kigamboni akieleza kwa hisia kali leo jioni ndani ya Bunge wakati wa majadiliano ya hotuba ya makadirio ya wizara ya ardhi, aliainisha msimamo wa wananchi wake, na kusema atakuwa wa kwanza kuunga mkono hatua za “kuufukuzia” mbali mpango huo kama serikali itakuwa haijajipanga kuhusu mradi huo. Pia, aliionya wizara hiyo kwa tabia za kukiuka sheria za umiliki wa ardhi kwa kuvamia na kuyatwaa maeneo ya wananchi bila kuwasiliana na serikali za mitaa husika, na pia kuficha baadhi ya viwanja vya mradi na hivyo kusababisha mapori kwenye maeneo yaliyopimwa, ambapo vibaka hutumia maeneo hayo kufanya uhalifu wa wapiti njia na wakati mwingine kuvamia nyumba za wakazi. 
  
Mwisho aliomba wabunge wamuunge mkono katika kupinga kupitishwa kwa makadirio ya wizara hiyo kama haitatoa ufafanuzi wa uhakika kuhusu matatizo ya wakazi wa Kigamboni. 
 

2 comments:

Simon Kitururu said...

Mmmmmh!

Upepo Mwanana said...

Tatizo ni kuwa serikali imekuwa inatoa amri nyingi za kiubabe wakati yenyewe haijajipanga. Wananchi wana haki ya kuja juu