Member of EVRS

Wednesday, 17 August 2011

Tanzia: Profesa Karashani Hatunaye tena

Taarifa ya kusikitisha imetufikia ya kuwa Prof. Karashani (Pichani juu) amefariki ghafla kwa mshtuko wa moyo usiku wa kuamkia jumapili nyumbani kwake Jijini Lusaka, nchini Zambia.

Mpaka mauti yanamkuta, Prof Karashani alikuwa mkuu wa Kitivo cha elimu ya anatomia (Anatomy) katika Chuo Kikuu cha Zambia (UNZA).
Katika safari yake ya kikazi, Prof Karashani alishawahi pia mkuu mkuu wa idara kama hiyo katika chuo kikuu cha Dar es Salaam kwenye kitivo cha tiba sehemu ya Muhimbili.

Sekta ya afya imempoteza nguli mmojawapo.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amen.

2 comments:

SIMON KITURURU said...

R.I.P Prof. Karashani !

Swahili na Waswahili said...

R.I.P Prof,Karashani na pole sana familia, Mungu awepe uvumilivu katika wakati huu mgumu.